Mwenyekiti wa NURU FOUNDATION Mama Zainab Kombo Shaib, amesema jamii inajukumu kubwa la kuijua na kuienzi thamani ya watoto yatima.


Mama Zainab ambayepia ni Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo jioni ya Julai 16, 2022, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar, akizungumza katika kikao cha tathmini ya hafla ya Dua ya kuiombea Nchi na Dhifa ya Chakula cha Mchana kwaajili ya Watoto yatima iliyofanyika siku ya sikukuu ya Iddi pili ya Mfunguo tatu.


Mama Zainab amesema dhamira kuu ya taasisi hio nikuwasaidia watoto yatima na jamii kwa ujumla na sio kujinufaisha kiuchumi.


"Wapo watu wasio waaminifu wanatumia mwevuli wa Mtoto yatima kama njia ya kujinufaisha kiuchumi, lakini katika taasisi yetu ya Nuru hilo halipo na sitokubali liwepo kabisa" alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Nuru Foundation.


Aidha ametoa wito kwa wahisani mbalimbali na jamii kwa ujumla, kuendelea kuisaidia taasisi hio ambayo ina idadi kubwa ya watoto yatima na wenye mazingira magumu ambao wanahitaji huduma za kila siku.


Wadau mbalimbali wa kikao hicho wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Taasisi ya MUZDALIFA Bwana Farouk Hamad Khamis, wametoa maoni yao ambayo yalionesha dhamira ya dhati ya kuunga mkono na kuendeleza juhudi za taasisi hio.


Hivi karibuni Taasisi ya Nuru kwakushirikiana na taasisi mbalimbali ilifanya hafla ya Dua na Dhifa ya Chakula cha mchana kwaajili ya watoto yatima, katika viwanja vya Mau se Dong na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wakiwemo watoto yatima kutoka katika mikoa mitatu ya kisiwa cha Unguja, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi.










Kitengo cha Habari NURU FOUNDATION

Julai 16,2022.

Share To:

Post A Comment: