Na Mwandishi Wetu.Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC, unaendesha mafunzo ya siku 2 ( julai 12 - 13 2022 )  kwa waandishi wa habari, takribani 45 kutoka Tanzania bara na visiwani. 

Mafunzo haya yamejikita katika kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu namna bora ya kuendana na sheria na taratibu mbali mbali zilizowekwa na serikali katika kuvisimamia vyombo vya habari, pamoja na mbinu za kuripoti maswala ya haki za binadamu.


 Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Albert Msando akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili kwa wanahabri kuhusu namna Bora ya kutoa habari hasa za Haki za Binadamu ambayo yameratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania -THRDC

Akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo hayo  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amewataka wanahabari kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ueledi zikiwemo za utetezi wa Haki za binadamu Ili kuongeza tija katika kuwahabarisha wananchi taarifa zilizojitokeza na zitakazojitokeza.

Msando amesema hayo leo Mkoani Morogoro wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari kuhusu namna Bora ya kutoa habari ambayo yameratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania -THRDC

Aidha Mkuu huyo Wilaya amewataka wanahabari kujitahidi kuwa watetezi wa Haki za Binadamu bila ya kuwa mashabiki wa kuegemea upande mmoja ili kuepukana na changanoto mbalimbali.

Amesema waandishi wa habari wanapozungumza Masuala ya Haki za Binadamu wasiwe wazito kwa kutozitoa badala yake waangalie mzani na ukweli katika kuhabarisha umma Juu tukio wanalotaka kuliripoti.

Naye Mhe jaji Mstaafu Robert Makaramba ( watatu kutoka kulia ) amewasilisha mada ya wanahabari namna ya kuandika na kuripoti habari za kwenye mahakama kuwa ni vyema wakaepuka kutoa taarifa ambazo hazijatolewa mahakamani ili kuepusha sintofahamu kwenye jamii.


Share To:

Adery Masta

Post A Comment: