Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Nungwi Zanzibar kupitia Chama cha Demokrasia Makini, Hussein Ramadhan Layya maarufu Msokolo.


 

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

 

ALIYEKUWA  Mgombea ubunge jimbo la Nungwi Zanzibar kupitia Chama cha Demokrasia Makini, Hussein Ramadhan Layya maarufu Masokolo amejitoa katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Msokolo akizungumza na waandishi wa habari alisema amechukua uamuzi huo baada ya kutafakari mwenendo wa chama chake ambao hautowi mwelekeo wa kukiimarisha chama kuanzia ngazi za chini.

Alisema wakati yupo katika Chama cha Demokrasia Makini  dhamira yake kubwa ilikuwa ni kuisadia jamii na kikiimarisha kwa kutatua kero mbalimbali.

Msokolo amesema mfumo wa kisiasa ulivyo sasa nchini unaifanya CCM kuwa na tofauti kubwa na vyama vingine vya siasa na ndio maana kimekuwa kikipata matokeo mazuri kila uchaguzi mkuu unapofanyika.

Alieleza kushangazwa kuona kwamba ndani ya Chama cha Demokrasia Makini tangu umalizike uchaguzi mkuu wa 2020 hakijawahi kukaa kufanya tathimini kama ambavyo CCM imekuwa ikifanya ili kubaini ni wapi walikosea hadi wasipate matokeo mazuri.

 Aidha, Msokolo alizindua tawi katika jimbo la Nungwi ikiwa ni historia ya chama hicho kuasisi tawi eneo lenye upinzani mkubwa ambapo aliweza kuvuna kundi kubwa la vijana wazee na kinamama kujiunga na chama hicho.

"Pamoja na kazi kubwa niliyoifanya kukiimarisha chama nilipoona sipewi ushirikiano nikaona ni nafasi yangu ya  kurudi ccm ambapo anaamini kwamba kuna ushirikishwaji mzuri katika ngazi zote kuanzia shina,tawi,wadi,jimbo wilaya,mkoa,hadi taifa," alisema Msokolo.

Msokolo kurudi CCM kuna tija gani,ni mtu mwenye kundi kubwa la watu wanaoamini kwamba anao uwezo mkubwa wa kuwasaidia na kuisaidia jamii kwa ujumla.

Msokolo pia ni mtu aliyejifunza mengi katika nchi mbalimbali na mwenye vipaji tafauti,kama vile sanaa ya uigizaji,uchoraji,uandishi wa habari,dereva,fundi seremala,mtunza ubora,msimamizi wa manunuzi,mtunza stoo na meneja usafirishaji.

Kama CCM  wakimtumia ipasavyo watakuwa wamelamba karata yenye thamani,na isitoshe katika kipindi hiki alichorudi ni wakati muafaka wa kuchukua fomu na kugombea nafasi yoyote katika chama kwani anao uwezo mkubwa na ni mbobezi katika laaluma tofauti na medani ya siasa.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: