Watanzania wametakiwa kukataa kudanganywa kuhusu zoezi la

sensa kwa sababu ni kitu ambacho kinatambuliwa na dini zote.


"Anayekuambia kuwa dini hairuhusu sensa au ni mambo ya dhambi

anakudanya . hivyo kuanzia leo hadi siku ya sensa mtu asikudanganye

kuhusu sensa," amesema Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo

Mnzava wakati wa ziara yake ya  kukagua miradi ya

maendeleo na kusikiliza kero mbalimbali na kuzitatua,


Mnzava amesema suala la kuhesabiwa ni muhimu sababu Serikali haiwezi

kutengeneza mipango ya maendeleo kwa wananchi wake bila kuwa na takwimu sahihi za wakazi wa eneo husika.


Akitoa mfano wa suala la sensa linavyoyambulika katika dini alisema

kwa Wakristo Yesu alizaliwa katika hori la ng'ombe wakati akienda

Bethlemu kuhesabiwa. Pia litoa hadithi ya Mtume Muhamad (SAW)

ambapoaliema wakati alipokufa aliwaacha waumini na mahalifa wanne.

Abubakari,Omari,Athimani na Ali


Amesema kuwa kati ya mahalifa hao mmoja alipopata malalamiko kuwa

watu hawatendewi sawa aliaimrisha  ifanyeike sensa ili ajue idadi

halisi ili watu waweze kuhudumia kwa usawa.Akifafanua, Mzava  alieleza  kuwa lengo la sensa hiyo ni kuisadia

Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa

utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya

afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za

kimataifa.


Alisisitiza kuwa taarifa  za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za

wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi

matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa

mgawanyo wa rasilimali


Katika hatua nyingine Mbunge  huyo Alisema  ataendelea   kuihamasisha

jamii kwenye mikutano ya hadhara na  Vikao kwenye ngazi  ya Wilaya,

Kata, Vijiji na Vitongoji ambapo aliongeza kuwa watakapopita makarani

wa sensa hakikisheni mnatoa taarifa sahihi bila uoga .


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya

Watu na Makazi ifikapo mwezi Agosti mwka huu.


Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa

kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS),

ipo kwenye maandalizi ya kufanya Sensa hiyo.


Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada

ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka

2012.


Hivyo Sensa ya mwaka huu itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini

baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine

zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

Share To:

Post A Comment: