Raisa said,Korogwe
MBUNGE wa Korogwe Vijijini Mkoani Tanga Timotheo Mzava amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan Kwa kuwapatia shilingi bilion 3.8 Kwa akili ya Ujenzi wa daraja llinalounganisha kata mbili za Halmashauri ya Wilaya
ya Korogwe.
Ujenzi wa daraja hilo unatimiza ahadi yake ambayo aliyoitoa siku mbili kabla ya kuteuliwa kuwa Rais.
Akielezea kuhusu daraja hilo wakati wa ziara yake katika eneo hilo linapojengwa daraja hilo,
amesema kuwa
daraja hilo ni ukombozi.
Amesema kuwa mradi huo utachukua miezi 18 kukamilika na akamtaka
mkadarasi huyo aliyemtambulisha kwa jina la Nyanzi kuhakikisha mradi
huo unakwisha kwa wakati na ikiwezekana hata kabla ya miezi hiyo
iliyopangwa.
Mnzava alimsifia Rais Samia kwa kusikiliza kilio cha wananchi wa eneo
hilo ambao walikuwa wanapata tabu a kuvuka na kuhatarisha maisha yao
kutokana na mto uo kuwa na mamba wengi wakilazimika kuvuka kwa kutumia
boti.
Amesema akiwa pale alimwomba Mama Samia wakati huo akiwa Makamu wa
Raisi ambaye aliagiza kiwekwe kivuko cha muda kuwasidia wananchi
kuvuka katika eneo hilo.
Amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo ni pamoja ujenzi wa barabara kuweka
changarawe kutoka eneo la Kwasunga hadi katika daraja hilo.
Mkazi wa Majengo, Mswaha, Zuberi Mbwana amesema wamepoteza watu
wanofikia wanne kwa kuliwa na mamba. “Hata mimi nimeshadondoka na
pikipiki hapa.kuna pikipiki kama mbili zipo ndani ya hapo hivyo
ujenzi wa daraja hili ni nafuui kubwa kwetu,” alisema Mbwana.
Mkazi mwingine wa Mswaha Darajani, Miraji Athumani Msanga amesema kuwa
wananchi walikuwa wanapata tatizo na hata wanawake walikuwa
wanajifungulia hapo kutokana na changamoto ya daraja.
“hapa ni kama makao makuu ya mamba. Watu walikuwa wanaliwa na mamba hapa. Ukivuka tu ni kama wanakutamani wanakuja.
Watu walikuwa wanatozwa Sh 1,000 kuvushwa hapo katika kivuko lakini tangu ujenzi uanze naona hali inaanza kupungua,” alisema.
Naye Msimamizi wa mradi huo Joel Mkinga alisema walichelewa kuanza ujenzi kutokana mchakato wa kupata vibari .
“Tu memaliza kukusanya vifaa na ujenzi utakamilika Septemba, mwakakesho,” amesema.
Post A Comment: