Wadau wa riadha mkoa wa Arusha wakiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iraqhe mara baada ya kuzindua Mbio za msimu wa Pili wa Clock Tower Marathon Mapema Leo Jijini Arusha



Meza Kuu ikiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Ausha Maximilian Iraqhe na Mwenyekiti Izack Shoo Wakati wa hafla ya Uzinduzi wa msimu wa pili wa mbio za marathon  za Clock Tower Leo Jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud


Na Ahmed Mahmoud

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iraghe Amewataka Wakazi wa Jiji la Arusha kujitokeza katika mbio za marathon za Clock Tower zitakazofanyika Jijini hapa tarehe 7 mwezi wa nane Mwaka huu.


Ameyasema hayo wakati akizindua halfa ya mbio hizo  mbele ya waandishi wa habàri na kuwataka Wakazi hao wa Jiji la Arusha na mikoa jirani sanjari na kujitokeza katika mbio hizo kuendelea kuliweka Jiji hilo katika hali ya usafi ili kuwezesha Watalii na wageni kufurahia madhari yake.


Alisema kwamba kila mmoja akihamasisha zoezi la usafi kwa jamii yetu miji yetu itaweza kuongeza wageni wanaokuja kutembelea hivyo utalii huu wa Michezo ni sehemu Moja itakayosaidia kuongeza wigo mpana na kukuza vipaji vya mchezo huu wa riadha.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya riadha Arusha Izack Shayo na waandaji wa mbio hizo za clock Tower amesema mbio hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika mwezi wa nane tarehe Saba Mwaka huu.


Amesema Mwaka huu washiriki  wameongezeka hadi Sasa tuna washiriki 1000 tofauti na Mwaka Jana idadi ilikuwa washiriki 800 na huu ni msimu wa pili wa mbio hizi  kwani mbio hizi washiriki wamekuwa wakizifurahia kwa sababu ya maandalizi yake.


Awali akiongea katika hafla hiyo Afisa Habàri na Uhusiano wa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya NHIF ambao ni wadhamini Miraji Shekifu amesema kwamba wafayakazi wao zaidi ya 25 watashiriki mbio hizo kwa Lengo la kujenga Afya zao na kuwataka wananchi kujitokeza ili Kupambana na magonjwa yasio ya kuambukiza. 


Amesema kwamba Dunia na nchi yetu inakumbana na magonjwa yasio ya kuambukiza ikiwemo Shinikizo la damu sanjari na kisukari Kutokana na ulaji mbaya na kutofanya mazoezi ndio maana wao kama mfuko wameweka mazingira mazuri ya kutoa huduma za Afya hadi kwa wanafunzi kwa TSH. 54,000 ili kuweza kupata huduma za Afya. 






Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: