Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana kushoto akiwaonyesha maboresho yaliyofanywa na Serikali bandarini hapo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tanga iliyotembelea Bandari hiyo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika mradi wa kimkakati wa maboresho kushoto Mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu kushoto akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) na Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tanga Dastan Kitandula wakitembelea Flow Meters za Bandari
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Tanga wakionyeshwa namna Floor Meter zinavyofanya kazi
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni MNEC wa Mkoa wa Tanga Ratco
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana akizungumza kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Bandari ya Tanga
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana akizungumza kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Bandari ya Tanga
MNEC wa Mkoa wa Tanga Ratco akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga Dkt Aisha Kigoda akieleza jambo wakati wa ziara hiyo
MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Tanga Rasul Shandala akizungumza wakati wa ziara hiyo

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa ziara hiyo

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge akichangia jambo wakati wa ziara hiyo


Na Oscar Assenga,Tanga.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimempongeza Rais Samia Suluhu na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika Bandari ya Tanga ambao utawezesha kuijengea uwezo wa ufanisi.

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Dkt Henry Shekifu wakati wa ziara ya kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tanga ilipotembelea Bandari ya Tanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika mradi wa kimkakati wa maboresho ya Bandari hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea bandari hiyo Dkt Shekifu alisema katika kipindi kifupi cha miaka mitano hali imekuwa tofauti na miaka ya nyuma huku akieleza eneo ambalo wametembelea ni hapo walipo wapo kwenye gati ambalo kwenda chini ni mita 13 .

Alisema kwa sasa eneo la karibia mita 200 zimejengwa kutoka ukuta wa zamani kuja ndani ili kuweza kuruhusu meli kubwa ziingie ambapo zimetumika fedha fedha nyingi sana na zitakuwa na tija kutokana na Bandari kuwa lengo la Biashara.

Mwenyekiti huyo alisema faida ambayo ni kubwa itawezesha meli kubwa kuingia Tanga na zikiingia uchumi wa Tanga utapanuka na hivyo kuchochea maendeleo kwa mkoa wa Tanga na wananchi wake.

“Kwa kweli hapa kumefanyika kazi kubwa sana na tumsifu Rais Samia Suluhu,Serikali imefanya kazi nzuri na watendaji sisi kama chama tunaona wamewatenda haki na wamekuwa waaminifu katika kutekeleza wajibu wao”Alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa.

Alisema kwa sababu ukizungumzia Bandari unazungumzia uchumi mkoa wa Tanga sasa hapo itakuwa ni jicho na itafungua uchumi wa mkoa wa Tanga hatua ambayo itachochea kasi ya maendeleo na hivyo kuwainua kiuchumi.

Aidha alisema anaamini CCM wana kila sababu ya ya kusema wana uwezo wa kuongoza nchi na watahakikisha wanafanya kazi ya kutekeleza yake ambayo wanahaidi wananchi.

Hata hivyo alisema upanuzi huo na wingi wa mizigo itakayotoka hapo haitakuwa na mahali ya kuwekwa sasa wanaiomba serikali suala la kurekebisha barabara za kutoka Tanga Bandari kwenda nje ni muhimu sana na kuna bandari ambapo zitawekwa kontena Mwambani sasa zitakuwa ni nyingi kuzitoa nje ya mkoa sasa kama hauna barabara ya kuzitoa maana yake utachelewa kuwafikia wa wateja.

“Sasa hapa ndio kutakuwa ni Jicho mizigo itatoka hapa itapelekwa nchi nyengine zitaletwa hapa na kupakizwa kwenye treni na kupelekwa nchi nyengine na hivyo kuinua uchumi wa mkoa wa Tanga”Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge alisema suala la reli na Bandari ni jambo la Msingi kuhakikisha wanapata shehena za kutosha kwenye Bandari ya Tanga.

Alisema wanamshukuru Rais kwa fedha nyingi alizotoa bilioni 429.1 ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni Bilioni 172.3 na awamu ya pili Bilioni 256.8 ambazo zimewezesha maboresho makubwa kwenye Bandari hiyo ikiwemo ununuzi wa mitambo.

Mbunge Ulenge alisema lakini pamoja na hayo bila mikakati ya kuongeza shehena ina maana bandari hiyo bado itakuwa haifanyi vziru hivyo wanaomba Reli ya Tanga hadi Arusha ifanye kazi na hiyo imeshakarabiwa karibia kilomita 400 lakini mpaka sasa haijafanya kazi.

“Tunaiomba Serikali ihakikishe Reli ya Arusha hadi Tanga iweze kufanya kazi ili tupate shehena kutoka Arusha na Kilimanjaro ambao wanakimbilia Bandari ya Mombasa Kenya wakati kuna bandari ya Tanga”Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana alisema ili Bandari iweze kufanya kazi kwa ufanisi lazima uinganishwe na reli kwa sababu bandari mzigo unapokuja haiishii bandarini lazima uenda kwa wananchi.

Alisema kwamba njia rahisi ambayo sio ya gharama kubwa ni reli sasa kuna kipande cha reli kinachounganisha Bandari ya Tanga na reli kipo hakifanyi kazi sasa wao TPA wameamua kufanyia kazi ili kuweza kikifufua.

“Hii sio mara ya kwanza kama mnakumbuka hata bandari ya Mwanza waliwahi kutengeneza meli wakiamini kwamba Bandari ya Mwanza meli ikifanyia kazi Bandari itafanya kazi lakini pia nakumbuka miaka sita iliyopita waliwahi kununua injini za reli kwa ajili ya kuwezesha kutoa mizigo bandarini kuunganisha na reli hivyo tutalifanyia kazi hilo kwa muda mfupi mzigo utakaotioka uende kwa njia ya reli”Alisema

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: