Waziri wa maliasili na utalii,Balozi  Dkt Pindi Chana akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusu onesho la sita la Swahili International Tourism Expo-S!TE 2022 linalotarajiwa kuzinduliwa October 21 hadi 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Bodi ya utalii Tanzania TTB,Felix John akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha.

Na Pamela Mollel,Arusha

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inatarajia kuzindua onesho la Sita la Swahili International Tourism Expo-S!TE 2022 litakalohudhuliwa na waoneshaji na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 550 kutoka katika masoko ya utalii duniani ikiwa ni mwendelezo wa programu ya Royal Tour hapa nchini.

Akizungumza  na waandishi wa habari Mkoani Arusha,waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt Pindi Chana alisema kuwa onesho hilo litafanyika katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es salaam,Oktoba 21 hadi 23 mwaka huu.

Alisema onesho hilo litakuwa mahususi kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuonesha bidhaa mbalimbali za utalii likiwa na lengo la kutangaza na kukuza utalii nchini.

Alisema tangu kuanzishwa kwa SiTE mwaka 2014 ,kumekuwepo na mafanikio makubwa ikiwemo ongezeko la waoneshaji na wanunuzi wa kimataifa ambapo mwaka 2014 hadi 2019 waoneshaji waliongezeka kutoka 40 hadi 170,huku wanunuzi wa Kimataifa wakifikia 333 kutoka 24

"Baada ya dunia kukumbwa na athari za janga la ugonjwa wa UVICO-19 mwaka 2019, serikali ililazimika kusitisha onesho hilo kwa muda"alisema.

Hata hivyo serikali ilichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuinusuru sekta hiyo ya utalii,na jitihada hizo zimewezesha kurejeshwa upya kwa onesho hilo.

Waziri Chana alisema kuwa onesho hilo litawahusisha watangazaji wa bidhaa mbalimbali za utalii,jukwaa la uwekezaji,semina kuhusu masuala ya utalii, masoko pia mikutano ya wafanyabiashara wa bidhaa za Utalii.

Alisema kuwa onesho la SiTE litakwenda sambamba na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya utalii ya mwaka 1999 ,pamoja na mkakati wa mwaka 2020-2025 wa kuitangaza Tanzania Kimataifa kuhusu utalii.

Alisema onesho hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano awanu ya tatu (FYDP III 2021/22-2015/26 ambapo zao lanutalii wa mikutano limeainishwa kama zao la utalii la kimkakati kwa lengo la kufikia watalii milioni tano na kufikia mapato ya dola za kimarekani bilioni 6 ifikapo 2025.

Awali kaimu mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB,Felix John alisema kuwa bodi yake imeshakamilisha maandalizi yote ya onesho hilo na kuwataka wadau wachangamkie fursa hiyo.

Aliongeza kwa kuwataka wadau wa utalii kutumia onesho hilo katika kuandaa vyakula vya asili kwa sababu watakao hudulia watapenda kuona vyakula vya tamaduni za kitanzania .
Share To:

Post A Comment: