Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepanga kuimarisha sekta ya bandari na sekta ya anga ili kukuza biashara ndani ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Rais Samia amesema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) yenye urefu wa kilomita 42.4. ambayo imegharimu shilingi Bilioni 197. 4.

Aidha Rais Samia amesema barabara hiyo ni muhimu kwa nchi ya Tanzania kwa kuwa ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha kanda ya Kaskazini (Northern Corridor) hadi Holili Taveta mpakani mwa Tanzania na Kenya kuelekea Voi nchini Kenya. 


Amesema barabara hiyo pia inaunganisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Kanda mbalimbali zinazounganisha Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia Sudani Kusini na Sudani hadi Ethiopia.

Vile vile Rais Samia amesema kukamilika kwa barabara hiyo kumeimarisha sekta ya utalii pamoja na ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii katika mikoa inayopita, nchi kwa ujumla, pamoja na nchi jirani.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: