Arusha

Jamii ya kifugaji wilayani Longido imetakiwa kuweka mikakati ya upatikanaji wa chakula shuleni kwa lengo la kuimarisha afya za wanafunzi pamoja na kuongeza ufauli wa masomo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi chakula katika Tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido,Mkurugenzi wa shirika la World vision Tanzania,Gilbert Kamanga amesema wametoa chakula kupitia mradi wa Ketumbeine AP kutokana na janga la njaa lililosababishwa na ukame kwa kipindi kilichopita.

"Ni vyema wazazi mkaanza mikakati sasa hivi ya upatikanaji wa chakula shuleni ili mradi huu utakapoisha watoto waendelee kupatiwa chakula shuleni kwani inasaidia kupunguza idadi ya utoro shuleni,"alisema Kamanga 

Kamanga chakula kilichotolewa ni takribani tani 117 za mahindi na tani 37 za maharage pamoja na mafuta ya kupikia ndoo 307  zenye ujazo wa lita 20 kila moja vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya sholkngi milioni 227.3 ambapo wanufaika wa msaada huo wakiwa ni watoto 10,272 kutoka shule za msingi 24.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ketumbeine Felix Mungaya amesema utoro wa wanafunzi umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwepo wa chakula shuleni kwani imewaletalea tija hata katika ufundishaji na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Naye mwanafunzi wa shule ya msingi katika shule hiyo, Kaleb Israel amelishukuru shirika hilo kwa kuwaboreshea miundombinu ya shule ikiwemo matundu manne ya vyoo na bafu,kisima kimoja cha kuhifadhia maji,bweni moja la wavulana lenye uwezo wa wanafunzi 72,Vitanda 50 pamoja na magodoro 100.

Aidha vitu vingine ni pamoja na Simtank mbili zenye ujazo wa lita 5000 kwa kila moja pamoja na madumu matano kwa ajili ya kunawia mikono kwa lengo la kujikinga na magonjwa mbalimbali ya milipuko.



Pia alisema shirika la World vision Tanzania limekuwa likiwasaidia kuwapa mafunzo ya kujitambua ili kuepuka mimba za utotoni,madhara ya ukeketaji pamoja na haki za watoto.



Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Longido,Boniphace Lugola alisema shirika hilo limkuwa msaada katika jamii hiyo ya kifugaji  pamoja na kufufua maendeleo katika Tarafa hiyo lengo ni kuinua uchumi wa wananchi mmoja mmoja na hata wilaya kwa ujuma.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: