Kaya zaidi ya 280 zilizobomolewa nyumba zao za kuishi na Biashara katika barabara ya Mianzini- Timbolo zimeamua kumwangukia Rais Samia Suluhu Hassan awasaidie kupata haki yao ya fidia ya shilingi Bilioni 1.7 baada ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kutoa hukumu wananchi hao walipwe kwa kuwa nyumba zao zilikuwa nje ya barabara na Halmashauri ya Arusha imekuwa ikikadi amri ya Mahakama.

Akizungumza na waandishi wa Mtandao huu katika eneo la tukio la uvunjwaji nyumba Mwenyekiti wa wananchi hao,Fanuel Titus Lamai ambaye ni Mwenyekiti wa Wahanga alisema walivunjiwa nyumba kutokana na kupanuliwa kwa barabara lakini Mahakama ilisema katika hukumu zake kuwa barabara ilifuata watu hivyo wananchi hao wanapaswa kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo.

Lamai alisema Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha wakati huo ,Jaji Fatuma Masengi na Majaji watatu katika Mahakama ya Rufaa walieleza wazi katika maamuzi ya hukumu zao kuwa wananchi hao wanapaswa kulipwa fidia kwa kuwa nyumba zilikuwa nje ya sheria ya barabara hivyo barabara iliwafuta watu na wanapaswa kulipwa fidia.

“Tunamwomba Rais Samia itusaidie tupate haki yetu kwa kuwa tangu mwanzo tunashinda kesi ila Viongozi wa Halmashauri ya Arusha wamekuwa na  shida kwenye utekelezaji wa amri ya mahakama.

“Tunaomba atusaidie tulipwe pesa zetu kwa  kuwa ni haki yetu kwani baadhi yetu wamekufa kwa mshituko na wengine wamepooza mwili na hawajui la kufanya na wengine walikopa benki kujenga nyumba za kuishi na biashara sasa wako taababi kimaisha hawajui la kufanya’’alisema Lamai

Akizungumzia sakata hilo, alisema ilikuwa mwaka 2011 walipewa taarifa na halmashauri ya Arusha, kuvunja nyumba zao kando kando ya barabara kwa kuwa barabara ilitakiwa.

 


 


 

Share To:

Post A Comment: