Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki EALA Fatuma Ndangiza akiongea na wanahabari hawapo pichani Leo Jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud 

Na Ahmed Mahmoud


Bunge la Afrika Mashariki limewapongeza na kuwaenzi Hayati Spika Mstaafu wa Bunge la Uganda Hayati Jacob Oulanya na Hayati Rais Mstaafu wa Kenya  Mwai Kibaki kwa kudumisha demokrasia na utawala bora.

Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Afrika Mashariki Fatuma Ndangiza amesema kwamba ipo haja kwa Bunge hilo japo hakuna sheria ikawekwa ili kuendelea kuwaenzi viongozi mbalimbali wa mataifa ya EAC kwa kujenga Utamaduni huo.

Amesema kwamba ukiangalia nchi ya Kenya imekuwa ikisifika kwa katiba bora,hapa utaona mchango mkubwa uliotolewa na Hayati Mwai Kibaki kujenga Demokrasia Wakati wa uongozi wake. 

Alisema viongozi hao ni wakupigiwa  mfano na kuendelezwa kwa Bunge hilo kuendelea kuwaenzi kukumbuka mchango wao kwa Taifa lao na mataifa ndani ya Jumuiya.

"Mwai Kibaki alianzisha Katiba na kutoa mchango mkubwa ili nchi iwe na katiba Sasa hivi miongoni mwa katiba ya viwango ni ya Kenya hii inasaidia nchi kuwa na Amani" alisema Ndangiza.

Alisema Bunge hilo linahitajika kuendelea kujenga Utamaduni huo kiwa endelevu kukumbuka viongozi wetu kwa wabunge kuleta muswada ili iingie kwenye sheria za Jumuiya yetu.

Alisema kwamba Hayati Spika Jacob alisaidia nchi yake kujenga demokrasia alitoa mchango kwa jamii kuwasaidia wenye maisha ya chini na yatima na kuendeleza domokrasia hili litawasaidia vijana.

Alisema kwamba Jamii zetu katika nchi za Jumuiya yetu zijenge Utamaduni wa kuwaenzi viongozi waliotenda. makubwa na kujenga misingi ya ukombozi demokrasia na utawala bora kwenye nchi za jumuiya. 

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: