Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Awali Zanzibar Mh. Ali Abdulgulam Hussein,akiteta jambo na Mhadhiri Msaidizi na Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano na Masoko Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Bw.Eusebius Mwisongo (kulia) baada ya kupita katika Banda la Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa maonesho ya tatu ya elimu ya juu yanayoendelea katika viwanja vya Mapinduzi Square, Michenzani Zanzibar. Kushoto ni Mhadhiri Msaidizi na Afisa Udahili wa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Samuel Marandu.


Mhadhiri Msaidizi na Afisa Udahili wa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Samuel Marandu,akitoa maelezo kwa wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Dk.Salmin waliotembelea Banda la Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa maonesho ya tatu ya elimu ya juu yanayoendelea katika viwanja vya Mapinduzi Square, Michenzani Zanzibar.

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kinatoa kozi mbalimbali kama ifuatavyo:

1) Master of Official Statistics 2) Master of Science in Agricultural Statistics 3) Postgraduate Diploma in Official Statistics 4) Postgraduate Diploma in Agricultural Statistics 5) Bachelor Degree in Official Statistics 6) Bachelor Degree in Data Science 7) Bachelor Degree in Business Statistics and Economics 8) Bachelor Degree in Agricultural Statistics 9) Diploma in Statistics 10) Certificate in Statistics.

Online application link : olap.eastc.ac.tz
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: