Na,Jusline Marco:Simanjiro

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa afya na usalama wa wachimbaji ni kitu cha kwanza kwa serikali hivyo ni vema wamiliki wa migodi wakazingatia taratibu na sheria za uchimbaji  ikiwemo kuajiri wataalamu wa baruti ili kuondokana na ajali zinazoweza kutokea kutokana na uzembe.


Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa  wachimbaji wadogo kuhusu usalama, utunzaji wa mazingira na usimamizi wa baruti migodini, mafunzo  yaliyofanyika katika mji wa Mererani wilayani Simanjiro ambapo alisema kuwa pamaoja na ongezeko kubwa la maduhuri katika sekata ya madini bila usalama wa wachimbaji haitaleta maana kwani  kumekuwa na matukio ya ajali kutokana na matumizi mabaya ya baruti.


“Siku za karibuni 2021/2022 tumepata matukio kama nane ya ajali katika eneo la machimbo haya ya Mererani na ajali mbili zimetokana na usimamizi mbaya wa matumizi ya baruti hivyo tumeona hatuhitaji kuendelea na madhara haya ndio maana tumekutana ili kupata mafunzo Kuhusiana na sheria za madini, usimamizi wa baruti, uchimbaji salama pamoja na utunzaji wa mazingira,”Alisema mhandisi Samamba.


Kuhusiana na suala la sensa ya watu na makazi Mhandisi Samamba aliwasisitiza wamiliki wa migodi na wote katika sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika zoezi Hilo ikiwa ni pamoja na kujaza dodoso linalohusiana na sekta hiyo ili kuweza kupata takwimu sahihi itayosaidia kufikisha huduma mbalimbali kwao lakini kutatua changamoto zinazowakabili.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dkt.Suleiman Serera alisema kuwa kama wilaya wameendelea kujipanga na kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto zinazojitokeza lakini pia kuendelea na ujenzi wa jengo linalohitajika ambapo fedha zake zimeshatolewa na ujenzi unaanza wiki ijayo.Wille Mpangilana meneja wa migodi ya Simon Kaijage block D alieleza kuwa kutokana na mwitikio mkubwa walio wamiliki, mameneja na walipuaji wa baruti  uonesha kuwa baada ya kutoka katika mafunzo hayo kutakuwa na mabadiliko makubwa katika utendaji wao wa kazi zao katika migodi kwa maslahi yao binafsi, jamii na nchi kwa ujumla.Share To:

JUSLINE

Post A Comment: