Na  Mwandishi wetu,Chunya

HALMASHAURI ya wilaya Chunya mkoani Mbeya  imesema kuwa kumekuwepo na ushirikiano  mkubwa  na mbunge  wa jimbo hilo ndo sababu ya msingi  ya  kufanikiwa kwa vitu vyote vya maendeleo ikiwemo ukusanyaji mapato ya halmashauri.

Kauli hiyo imetolewa mswishoni mwa wiki na Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya Chunya ,Tamimu Kambona wakati akizungumza timu ya waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mbeya waliofika katika wilaya hiyo kuangalia shughuli mbali mbali za kimaendeleo .

Kambona amesema kuwa uwepo wa viongozi wa kisiasa akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo ,Masache Kasaka ,madiwani  na viongozi wengine wamekuwa msaada mkubwa katika wilaya hiyo katika kuhakikisha wilaya hiyo inasonga mbele kimaendeleo hususani katika ujenzi wa shule za sekondari ,ukusanyaji mapato,ujenzi wa jengo la madini ,afya na vitu vingine vya maendeleo.

“Ndo maana unaona Chunya imetulia vizuri na si kwa Chama cha mapinduzi tu bali mpaka vyama vingine kote kuna ushirikiano  mzuri ambao unapelekea wilaya yetu kusonga mbele,tunashukuru wilaya yetu kuwa na utulivu ila tunayemshukuru Mbunge wa jimbo la chunya amekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha chunya inakuwa katika hali ya utulivu ’amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Masache Kasaka amesema kuwa kwa kushirikiana na halmshauri amekuwa akiwakilishwa na Katibu wake kuangalia changamoto mbali mbali ambazo zinakuwa zimetokea katika maeneo hayo na kuzipatia ufumbuzi.


Share To:

Post A Comment: