Na Raphael Kilapilo 


Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Eng. Victor Seff ametoa mwezi mmoja kwa TARURA Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi kukamilisha ukarabati wa Daraja la Ifume.


Eng. Seff ametoa maagizo hayo leo Mei 17, 2022 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya barabara katika Mkoa wa Katavi.


“Daraja hili ni muhimu sana kwa wakazi wa hapa kwa shughuli za kiuchumi, hivyo ni lazima mhakikishe kazi hii inakamilika kwa haraka ili wananchi wa kalamsenga na Itunya waweze kusafirisha mazao yao bila kupata usumbufu unaojitokeza kwa sasa, “ alisema Eng. Seff.


Alisema kuwa TARURA Makao Makuu itatoa fedha ambazo alielekeza zitumike katika ukarabati wa Daraja hilo, na aliagiza tathimini ifanyike haraka na maombi ya fedha hizo yatumwe ili yafanyiwe kazi kwa haraka.

 

Pia aliwaagiza TARURA wilaya kuhakinisha wanatoa kwa haraka magogo na uchafu wote ulioletwa na mvua na kusababisha kuziba kwa daraja hilo ili fedha zikija ukarabati ufanyike ndani ya muda wa mwezi mmoja aliotoa.


Naye diwani wa kata ya Kapalamsenga Mhe. Jefu Lameki alisema kuwa anaushukuru uongozi wa TARURA  kwa kusikia kilio chao Kwani wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na kuharibika kwa daraja hilo, na alieza kuwa wanachi watashiriki kikamilifu kuondoa magogo na uchafu katika daraja.


Aidha Eng. Sef alikagua ukarabati wa barabara ya Kapalamsenga - 

Ifume kuelekea bandari ya kareme, Tanganyika yenye urefu wa km 12.1 na kuridhishwa na kazi inavyoendelea, ambapo mpaka sasa ukarabati umefikia asilimia 90.


 “ Barabara hii Itasaidia sana katika shughuli za usafirishaji wa mazao na pembejeo  za kilimo na  ni sehemu ya barabara ya kutokea bandari ya Karema hivyo ni barabara muhimu sana,” alisema Eng. Seff


Share To:

Post A Comment: