Na;Jusline Marco;Arusha


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali inaendelea kufanya mapitio juu ya mkopo wa elimu ya juu kuona ni kwa namna gani mikopo hiyo itaweza kuwanufaisha na wanafunzi wanaosoma elimu ya kati.


Majaliwa ameyasema hayo Mei  24 wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la ufundi Tower lililopo katika Chuo cha Ufundi Arusha,ambapo alisema serikali  imejikita kwenye utoaji wa mikopo kwa shahada hivyo wakati umefika wa kuona namna ya kuboresha  elimu ya kati ili vijana hao waweze kunufaika zaidi kupitia mikopo inayotolewa na serikali.


Ameeleza ameeleza kuridika na ujenzi wa jengo la Ufundi Tower linalojuisha maabara, madarasa,pamoja na  Kliniki itakayo wahudumia watumishi,wanafunzi na wananchi wa Arusha walio karibu na chuo hicho ambapo ameahidi kuwa wataendelea kuleta fedha za ujenzi katika chuo hicho ili kupunguza changamoto ya mabweni.


Aidha amefafanua kuwa serikali imetoa fedha za kutosha kwenye sekta ya elimu  kwanzia chekechea kwa wanafunzi wa kawaida wenye mahitaji maalum ambapo kwa sekondari wameanza kwa ujenzi wa madarasa na sasa wanajenga mabweni ili kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi wa kike na wakiume.



Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt.Mussa Chacha katika hafla hiyo amesema ujenzi wa jengo hilo ulioanza Julai 2021 baada ya kupokea kiasi cha fedha shilingi bilioni 1.449 kama ruzuku ya fedha za maendeleo kutoka serikali kuu kwa ajili ya bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 428 ambapo lengo la mradi huo ni kuongeza fursa na idadi kwa wanafunzi wa kike katika fani za ufundi.


"Mradi huu umefikia asilimia 72 ya utekelezaji na unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agust mwaka huu na unatekelezwa kwa njia ya force account kupitia wataalam wa ndani."alisema Dkt.Chacha


Sambamba na hayo Dkt.Chacha amesema kazi ya umaliziwaji wa ghorofa 3 inayojumuisha madarasa,maabara na ofisi,chuo cha Ufundi Arusha ilipokea jumla ya shilingi bilioni 1.751 kutoka serikali kuu kipitia program ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19,ambapo mradi huo umefikia asilimia 88 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.


Katika ujenzi wa Kliniki ya Tiba,Dkt.Chacha amesema jumla ya fedha shilingi bilioni 1.036 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kliniki hiyo inayolenga kuboresha utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi anaosoma program ya vifaa tiba ambapo ni mpango wa chuo hicho kupunguza utegemezi wa nchi kuagiza vifaa tiba nje ya nchi kwa kutengeneza vifaa hivyo.


"Wataalam wameanza matayatisho ya kutengeneza prototypes za automated mikono ya bandia,mashine za kutunzia watoto njiti na kliniki hii itatoa huduma ya afya kwa wanafunzi,wafanyakazi na jamii ya mkoa wa Arusha."Aliongeza Dkt.Chacha


Aidha katika risala yake hiyo Dkt.Chacha amesema chuo hicho kilianzishwa mnamo mwaka 1978 chuo kilipewa jukumu la kutoa mafunzo ya ufundi sanifu katika ngazi ya cheti ambapo mpaka sasa chuo kinatoa mafungo ya ufundi stadi kwa ngazi mbalimbali,elimu ya ufundi ngazi ya Astashahada,stashahada na shahada katika ya michepuo ya sayansi,teknoloji na ufundi.


Ameongeza kuwa pamoja na utekelezaji wa majukumu hayo chuo hicho kina majukumu mengine ya kufanya utalii na kutoa ushauri wa kitaalam kwa jamii ikiwa ni utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025,ilani ya uchaguzi mwaka 2020/25 na mpango wa tatu wa taifa wa maendeleo wa miaka 5 , mwaka 2020/21 hadi mwaka 2025/26.


Naye Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema uwekaji wa jiwe hilo la msingi ni matokeo ya jitihada kubwa ya serikali kuwezesha kufanya miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kupitia fedha za UVIKO 19 ambapo wizara ya elimu ilipata bilioni 64.9 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali.


"Fedha hizi zilielekezwa katika vituo vya veta 25 vya wilaya,vyuo 4 vya veta mkoa na vyuo vya ualimu kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia na zimeweza kurahisisha mazingira ya wanafunzi kukaa katika madarasa mna mabweni mazuri."alisem Prof.Carolyne


Amebainisha kuwa kupitia fedha hizo Wizara itaendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufjndishia ambapo pia wizara kmeahidi kuwa bega kwa bega na viongozi wengi kuhakikisha malengo ya serikali kupitia wizara ya elimu yanatimizwa.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: