Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akiongea kwenye Kikao Cha Kamati ya Maridhiano na dini mbalimbali pamoja na kamati ya Amani Mapema mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha 
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Arusha na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe akiongea kwenye Kikao Cha Kamati ya Maridhiano na dini mbalimbali pamoja na kamati ya Amani Mapema mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha 


Na Ahmed Mahmoud

Serikali imeeleza kwamba itaendeleza kushirikiana na kuwatumia viongozi wa dini na kimila ili kuifikia jamii ya watanzania katika kudumisha Amani na mshikamano wa watanzania.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe kwa Niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela kwenye kikao Cha viongozi wa dini na madhebu Mbalimbali kilichofanyika Jijini Arusha.


Amesema ili serikali iweze kuifikia jamii yote kunahaja ya kuendelea kuwatumia viongozi wa dini na madhebu mbalimbali kwa Lengo la kuhakikisha Elimu inaifikia jamii kwani viongozi hao wapo Karibu na jamii.


"Niwaombe viongozi wa dini na madhehebu yote kuisaidia serikali kutoa Elimu kwa jamii juu ya sensa ya watu na makazi sanjari na Anuani za makazi inayoendelea nchini kwa Sasa kwani mmnauwezo wa kuifikia kwa ukaribu"


Awali akiongea kwenye Kikao hicho Sheikh Alhad Mussa amesema ushirikiano uliopo kati ya serikali na makundi ya dini ni kuendelea kuwatumia ili kuweza kuisaidia jamii kupata uelewa masuala mbalimbali ambayo serikali inayataka kufikiwa kwa jamii.


Amesema kwamba wao viongozi wa madhehebu mbalimbali wataendelea kuhubiria wauumini wao suala zima la Amani umoja na maridhiano miongoni mwa watanzania katika kujenga kizazi kinachoheshimu maadili.


"Humu sisi tunayo makundi mawili kuna kamati ya Amani na Kamati za maridhiriano hizi zote zinaenda sawa wala hazihitajiki kuchanganywa hikima hii ipo hata kwenye vitabu vitakatifu hivyo tuhubiri Amani mshikamano na upendo miongoni mwa jamii zetu kwa kushirikiana na serikali yetu.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Kamati ya Maridhiano Kanda ya Kaskazini Sheikh Abdulrazak Amir amesema Lengo la kushirikiana baina ya kamati hizo ni kuendelea kujenga umoja mshikamano licha ya kutokuwepo na misuguano katika jamii zetu.


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: