Na Ahmed Mahmoud 

Mawakili na Wanasheria Vijana wametakiwa kujiunga katika makundi na kutumia fursa mbalimbali za kazi zao kwa kuanzisha ofisi Moja badala ya kila moja kuanzisha ofisi yake ili kuwasaidia kuongeza kipato na maendeleo kwa umoja.

Akizungumza na waandishi wa habàri Rais wa Chama Cha wanasheria nchini TLS Pro.Edward Hosea mara baada ya kujieleza Wakati akiomba kura kwenye uchaguzi wa TLS Jijini Arusha amesema kwamba yeye anaamini katika maendeleo,uwekezaji,ushirikiano na serikali ili kufikia malengo ya kiuchumi kwa chama hicho.

Amesema kwamba TLS atakayoongoza kwa kipindi Cha pili itawasaidia mawakili vijana kuweza kunufaika na kutumia fursa kwa kutumia ofisi zao 21 nchi nzima kuweza kujiinua kiuchumi kwa kutumia mpango Legal aid.

"Nimekuwa muumini wa Maendeleo na uwekezaji ndio maana nimekuwa Karibu na serikali sio kujipendekeza Badi kujenga hoja na ieleweke sio kuwekwa mfukoni Bali kukisaidia chama chetu kufikia malengo ya uwekezaji" 

Hata hivyo amebainisha kwamba mawakili vijana watumie fursa ya legal aid katika ofisi zetu 21 nchi nzima kuweza kupata kazi ambazo tuna makundi mbalimbali yanahitaji msaada wa kisheria ndio Lengo la kuanzisha ili kuwasaidia kukua kiuchumi.

"Mmeona tumezindua Wakili Sacco's tunahitaji kujitanua zaidi kuweza kuwekeza TLS ni Taasisi kubwa sana sisi huko tulipotoka Sacco's iliweza kutukomboa angalia Waalimu Wana vitega uchumi sisi ni tasnia kubwa tuwekeze katika vitega uchumi nchi za wenzetu Wana makampuni makubwa na hawategemei michango ya wanachama"

Kwa mujibu wa Prof.Hosea chama hicho kitaendelea kushirikiana kwa ukaribu na serikali kwa kuejnga hoja na kuachana na dhana ya uwanaharakati ambayo haijenga kwani nchi yetu ni muumini wa Amani hivyo sio busara kutojenga hoja katika Yale tunayoona hayaendi sawa.

Kwa Upande wake Mgombea wa Nafasi ya chama Cha wanasheria wa Afrika Mashariki na Makamu Mwenyekiti wa ZLS Shahazad amesema kwamba Msingi wa fursa zilizopo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ndio umemsukuma kugombea nafasi hiyo.

Amesema Tanzania haijanufaika sana na biashara ya mipakani ya kisheria kama walivyo wenzetu Kenya na Uganda hivyo huu Sasa ndio Wakati wa yeye kuweka mazingira mazuri ya kuongeza na kutumia fursa mbalimbali kwa kuziunganisha jamii na wanasheria wa Afrika Mashariki ili kuisemea changamoto zao kupitia nafasi hiyo.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: