Na;Jusline Marco;Arusha


Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii  Juma Mkomi amewataka makamisha wa shirika la hifadhi Tanzania (TANAPA) kuwa waadilifu katika utendaji kazi wao ili kuweza kulinda hifadhi hiyo.

Akizungumza katika hafla ya uvishwaji wa vyeo kwa makamisha wasaidizi wa uhifadhi  wa shirika hilo,Mkomi amesema kuwa ni vyema viongozi hao wakawa waadilifu kwenye kulinda hifadhi,rasilimali na katika kuwasimamia wenzao ambapo ameomba suala la uadilifu liwe kipaumbele.

Aidha ameongeza kwa kuwataka viongozi hao kutafuta namna bora ya kuwafanya wananchi kuweza kushiriki vya kutosha katika kupendekeza aina gani ya mradi wangenauoipenda ambayo itasaidia kuhakikisha miradi hiyo inawagusa moja kwa moja.

"Ili kuweza kulinda rasilimali hizo ziweze kuendelee kuwepo miaka na miaka na kuongeza kipato cha nchi jambo la msingi ni uhifadhi wa maeneo yao ili vivutio katika hifadhi visiweze kipoteza ubora."alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa maliasili na utalii

Naye Kamishna wa Shirika la hifadhi Tanzania,William Mwakilema katika hafla hiyo amewaelekeza viongozi hao wa uhifadhi kupitia majukumu yao kuwa umakini  kuyatekeleza ipasavyo na kuwasisitiza kutumia vipawa vyao, vipaji, uzoefu,elimu na busara katika kuwaongoza watumishi watakao kuwa chini yao.

“ Katika maeneo yenu ya kazi mnapaswa kuwa viongozi kwa kuonyesha njia, nendeni mkawaunganishea maafisa na askari mtakaowasimamia ili kutimiza malengo ya shirika na nchi kwa ujumla,” Alisema Mwakilema.

Pamoja na hayo aliwataka maofisa na maaskari wote kutoa ushirikiano wa kutosha ili makamishna hao wasaidizi wa uhifadhi walio teuliwa waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo lakini pia waweze kuendelea kujituma  na kutekeleza wajibu wao pamoja na kuimarisha nidhamu ndani ya jeshi, nidhamu binafsi na nidhamu kwa wengine.








Share To:

JUSLINE

Post A Comment: