Padre Athanas Mgimba kwa niaba ya  askofu jimbo  katoliki la Njombe akimwagia maji ya Baraka gari mpya ya kanisa lililokabidhwa kwa kanisa hilo.
Gari mpya kwa ajili ya kanisa Roman Katoliki Parokia ya Utalingolo iliyonunuliwa  kwa michango na waumini kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwa imesogezwa mbele ya kanisa hilo mkoani Njombe.


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 121 kimefanikisha ununuzi wa  gari jipya aina ya land cruser hard top kwa ajili ya utoaji huduma za kichungaji katika parokia ya Utalingolo jimbo katoliki la Njombe kutokana na kuwapo kwa changamoto ya uhaba wa vyombo vya usafiri.

Taarifa ya makabidhiano ya gari hilo katika kanisa hilo  iliyosomwa na katibu mkuu wa kamati ya uhamasishaji wa ununuzi wa gari hilo bwana Deogratias Mtewele imesema fedha hizo zimetokana na michango mbalimbali ya waumini,wadau wa maendeleo pamoja na wafadhili toka nje ya nchi.

“Kamati ya ununuzi wa gari ya parokia iliundwa mwaka 2019 mwezi septemba,na imeafanikiwa kununua hii gari mpya yenye tahamani ya shilingi milioni 121 laki tatu elfu 57 na 666 amabpo fedha hizo zilitokana na michango ya waumini na wafadhili wa ndani nan je ya nchi”alisema Deogratias Mtewele

Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji wa ununuzi wa gari hilo bwana Erasto Mpete ambaye ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe na diwani wa kata ya Utalingolo anasema haikuwa kazi rahisi kupatikana kwa chombo hicho cha usafiri .


“Gari hili litumike kwa ajili ya uinjilishaji na kumtukuza Mungu tuombe chombo hiki kitunzwe ili kiweze kutumika kwa muda mrefu”alisema Mpete

Kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deodatus Mwanyika katibu wa mbunge huyo Andreas Mahali anasema ushirikiano wa pamoja ndio unaowafikisha mbali wananchi kimaendeleo kama walivyoshirikiana kununua gari hilo.

Mwanasheria wa mkoa wa Njombe Hilmar Danda akimwakilisha mkuu wa mkoa anasema ni lazima serikali iendelee kuziunga mkono dini zote licha ya kuwa yenyewe haina dini.

“Lazima tufanye kazi kama timu ili tuweze kufanikiwa,tuepukane na ile ya kusema mimi nitafanya na tuseme sisi tutafanya na ndio maana Utalingolo leo hii mnafurahia matokeo hayo”alisema Mahali

Padre Athanas Mgimba kwa niaba ya  askofu jimbo  katoliki la Njombe anasema kila muumini wa kanisa katoliki Utalingolo anapaswa kuwa mlinzi wa gari hilo huku paroko wa parokia hiyo padre lukas mgaya ameshukuru jitihada zilizofanyika hadi kupatikana kwa gari hilo.

Share To:

Post A Comment: