N


a,Jusline Marco:Arusha


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzunduzi wa Filamu ya Toyal Tour utakao fanyika jijini Arusha Aprili 28 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema uzinduzi huo umelenga kuwavutia watalii na wawekezaji nchini.

Aidha amesema kuwa katika uzinduzi huo wanatarajia kuwa na wageni pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa,mabalozi ,wadau wa utalii na uhifadhi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Tanga pamoja na Manyara.

Ameongeza kuwa wastani wa watalii laki 5 na elfu 62,mia 549 waliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi kwa mwaka 2020 hadi kufikia watalii laki 7,elfu 88 na mia 933 kwa mwaka 2021 idadi hiyo ikiwa ni watalii wa ndani.

Vilevile amesema idadi ya watalii wa nche waliotembelea hifadhi mbalimbali nchini  imeongezeka kutoka watalii laki 6 ,elfu 20 mia 867  kwa mwaka 2020 na kufikia watalii laki 9, elfu 22 na mia 692 mwaka 2021.

"Tunaamini kuwa kupitia juhudi hizi za Mhe.Rais kama "Tour Guide"namba moja katika utengenezaji wa filamu hii itaendelea kuongeza chachu na muitikio mkubwa zaidi kwa wageni watakaotembelea nchi yetu."Alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha

Pamoja na hayo amewataka wananchi hususani wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kimpokea Mhe.Rais katika kuelekea kwenye uzinduzi huo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko kayika Ukkmbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha ICC, Mkunde Senyagwa Mushi, amesema wataandaa mazingira kulingana na viwango vya kimataifa ili uzinduzi huo uweze kwenda vizuri na kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi zote katika kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan.


Naye kamishna msaidizi wa utalii kutoka TAWA,Segoline Tarimo amesema wako bega kwa bega na Rais Samia katika uzinduzi wa filamu hiyo kwani, filamu hiyo imeleta matokeo chanya nchini na kuahidi kuimarisha miundombinu mbalimbali  ya utalii kwa ajili ya wageni.



 
Share To:

JUSLINE

Post A Comment: