Na Mwandishi Wetu.

Kwa wiki kadhaaa sasa Mtandao namba moja Tanzania kwa utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo Tanzania umekua ukiendesha promosheni ifahamikayo kama " PESA MWAA MWII NA TIGO PESA "

Ambapo takribani milioni 40 zimekua zikitolewa kila wiki kwa washindi 20 wa milioni mbilimbili kwa wiki nne mfululizo , na Leo Aprili 21 , 2022 Droo ya fainali imechezeshwa katika ofisi za Tigo makao Makuu Jijini Dar Es Salaam ambapo wamepatikana Washindi 10 wa milioni kumi kumi kila mmoja pamoja na mshindi mmoja mkubwa wa Milioni 25 .

Meneja wa wateja maalum Tigo Pesa Bi. Marry Rutha akichezesha Droo ya fainali ya Pesa Mwaa Mwii , kushoto ni mwakilishi kutoka bodi ya michezo Ya kubahatisha Bwn. Elibariki


Akizungumza baada ya kuchezesha droo hii ,Meneja wa Kitengo cha wateja Binafsi Tigo Pesa Bi. Mary Rutta  amewapongeza washindi wote ambao wamejishindia zawadi mbalimbali katika promosheni hii ya PESA MWAA MWII NA TIGO PESA na kuwasihi wateja wengine ambao hawakubahatika kushinda kuendelea kutumia Tigo Pesa maana kuna mambo mengi na mazuri yanakuja

" Kama ilivyo kawaida yetu Tigo Pesa hatujawahi kuishiwa  kutoa zawadi na mambo mengine mazuri kwa wateja wetu , kwahiyo niwasihi wateja wetu kuendelea kutumia huduma zetu maaana kutumia Tigo Pesa kunalipa " .



Suzani Assey Daniel , Mama Ntilie ( miaka 41 ) Mkazi wa Kigamboni jijini Dar Es Salaaam ameibuka mshindi wa milioni 25 Fainali ya Promosheni ya Pesa Mwaa Mwiii na Tigo Pesa .

Kutokana na furaha aliyokua nayo Suzan alishindwa kabisa kuzungumza  .

 Baadhi ya washindi 10 wa Milioni Kumi kumi kila mmoja ni Kalunde Ismail Fundikila ( miaka 28 ) Mkazi wa Kinondoni , Consolata Chissinka ( Miaka 29 ) mfanyabiashara wa mbao Njombe, 

Elvis Clemence ( miaka 28 ) mkulima Kilosa Morogoro , na Bi. Shamimu ( miaka 41 ) mjasiriamali Arusha.

Kumbuka walioibuka washindi kwenye promosheni hii ya PESA MWAA MWII NA TIGO PESA ni waliofanya miamala mara nyingi awezavyo kupitia huduma za Tigo Pesa ikiwa ni pamoja na Lipa Kwa Simu, Malipo ya Bili, Malipo ya Serikali, miamala ya mtandaoni kutoka kwa wenzao na kupokea pesa kutoka kwa mtandao mwingine wa simu .

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: