Dar es Salaam: Machi 16, 2022, Tigo kwa kushirikiana na Samsung Electronics Tanzania leo wametangaza kuzindua huduma ya mtandao wa nyumbani kwa watumiaji wa Smart TV. Televisheni zote mahiri za Samsung zinazonunuliwa katika maduka yaliyoidhinishwa nchini kote zitakua na ROUTER ya intaneti (CPE, MIFI) na kifurushi cha kila mwezi cha Intaneti bure. Tigo imedhamiria kuhakikisha

Dar es Salaam: Machi 16, 2022, Tigo kwa kushirikiana na Samsung Electronics Tanzania leo wametangaza kuzindua huduma ya mtandao wa nyumbani kwa watumiaji wa Smart TV. Televisheni zote mahiri za Samsung zinazonunuliwa katika maduka yaliyoidhinishwa nchini kote zitakua na ROUTER ya intaneti (CPE, MIFI) na kifurushi cha kila mwezi cha Intaneti bure.

Tigo imedhamiria kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata uzoefu wa maudhui ya kweli ya 4K kwenye mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ kwa kutoa intaneti bila malipo ya hadi GB 285 kwa siku tisini kwa mteja yeyote anayenunua modeli zilizochaguliwa za Samsung Smart TV.

Afisa Mkuu wa Ubunifu na Mikakati wa Bidhaa za Tigo, David Umoh

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hizo, Afisa Mkuu wa Ubunifu na Mikakati wa Bidhaa za Tigo, David Umoh, alisema, “Uzinduzi wa huduma ya Intaneti ya Nyumbani na Tigo kwa watumiaji wa Smart TV kwa kushirikiana na Samsung Electronics Tanzania ni wa kwanza wa aina yake nchini, na inaongeza wingi wa bidhaa na huduma za kiubunifu zilizoundwa na Tigo ili kutoa uzoefu wa haraka na wa kutegemewa wa broadband kwa wateja wetu kote Tanzania.”

“Kama mtoaji anayeongoza wa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania tunafanya kazi kila kuja na bunifu mpya katika kutengeneza ulimwengu wa kidijitali kwa wateja wetu, tunaamini kuwa kila nyumba inastahili kupata manufaa ya maisha ya kisasa yaliyounganishwa ambayo ndiyo nguvu inayosukuma kupitishwa kwa hii huduma.” Alisema Umoh.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki, Tae Sun Lee alisema kuwa “Kama Samsung tunaendelea kuboresha bidhaa zetu na tunaona inafaa tu kuwaleta washirika wetu katika safari hii ambayo tumeianza tena Tanzania. Uzinduzi wa ushirikiano huu wa kimkakati na Tigo unaimarisha zaidi dhamira yetu ya kuleta teknolojia bora kwa watu wanaotumia Samsung 4K Smart TV na Tigo. Tunatumai ushirikiano huu utasaidia kuleta matumizi bora kwa wateja”

Mtandao wa Nyumbani kwa Tigo unatoa hali ya kipekee ya mtumiaji kwa wateja wote wa Tigo, Suluhisho linalomlenga mteja linatoa uzoefu wa kidijitali usio na kikomo na utaongeza thamani kwa wateja huku wakitumia mtandao wa intaneti wa Tigo wenye kasi ya juu wa 4G+.

Wateja wanaweza kutembelea maduka yaliyoidhinishwa ya Samsung Electronics Tanzania ili kununua Samsung Smart TV na kupata MIFI au CPE bila malipo na hadi 285GB ili kupata maudhui ya kweli na muonekano angavu wa HD.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: