p>

Meneja wa Kituo cha Utafiti cha TARI Mikocheni Dkt.Joseph Ndunguru akifungua mafunzo hayo ya kitaifa ya siku nne kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TARI.
Afisa Programu ya CAADP -XP4, Bi. Futh Magagula akitoa salamu za Taasisi ya Uratibu wa Tafiti za Kilimo Afrika (CCARDESA) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es salaam.

Meneja wa Mawasiliano na menejimenti ya Maarifa kutoka Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) Dkt. Richard Kasuga akieleza malengo ya Mafunzo hayo ya Kiataifa ya siku nne kwa Maafisa mawasiliano, Wanahabari na wadau wengine.

Afisa Habari na Menejiment ya Maarifa kutoka kutoka Taasisi ya Uratibu wa Tafiti za Kilimo Afrika (CCARDESA) Bi. Bridget Kakulwa akieleza akieleza matarajio ya Mafunzo hayo.Bwana Shadrack Ndalawa msimamizi wa dawati la CAADP Wizara ya Kilimo akieleza utekeeleaji wa maazimio Malabo upande wa TanzaniaWashiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi. 

Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi.


 Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi.


Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi.

Mafunzo yakiendelea.

Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi.

Mafunzo yakiendelea

Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi.Na Calvin Gwabara – Dar es salaam.

MAAFISA Mawasiliano na Waandishi wa habari wametakiwa kutumia taaluma zao kufikisha matokeo ya tafiti na vumbuzi mbalimbali zinazozalishwa na watafiti nchini kwa Wakulima na wafugaji ili zisaidie kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili kuinua uchumi wa watu na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Meneja wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni Dkt. Joseph Ndunguru wakati akifungua mafunzo ya kitaifa ya siku nne ya kuwajengea uwezo Maafisa mawasiliano, Wagani na Waandishi wa habari namna ya kuchakata matokeo ya Tafiti na kuwafikishia walengwa sambamba na kufuatilia na kutoa taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Malabo ulioandaliwa na Taasisi ya Uratibu wa Tafiti za Kilimo (CCARDESA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

“Mafunzo haya ni muhimu sana kwa maafisa mawasiliano hawa kutoka vituo vyote vya utafiti nchini, Wizara ya Kilimo, Wizara ya mifugo na Uvuvi, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Mamlaka ya Hali ya Hewa pamoja na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari maana wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanatafsiri matokeo ya tafiti kwa lugha rahisi na kuwafikishia walengwa na kwa kufanya hivyo kutasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija na pia kusaidia kufikia malengo ya Maazimio ya Malabo” alisema Dkt. Ndunguru.

Aidha amefafanua kuwa kupitia mafunzo hayo kutawawezesha kujua Maazimio saba ya Malabo na hivyo kuchochea Serikali kutimiza malengo yake ya kutenga asilimia kumi ya Pato la taifa kuingiza kwenye kilimo na ushiriki wa wadau wengine katika kusaidia kuinua kilimo na kuinua uchumi wa jamii na taifa.

Dkt. Ndunguru amesema zaidi ya asilimia 55 ya Waafrika wamejiajiri kwenye sekta ya kilimo lakini bado kilimo hakijatoa  mchango unaokusudiwa katika kuinua pato la taifa na hii ni kutokana na sababu mbalimbali ambazo zingine tayari sababu hizo majibu yake yamepatikana kupitia tafiti za kisayansi lakini hazijawafikia walengwa.

Kwa upande wake Afisa Programu ya CAADP -XP4 kutoka CCARDESA Bi. Futh Magagula ameipongeza Tanzania kwa kuwa nchi ya kwanza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mwisho uliofanyika Afrika kusini kwa kufanya mafunzo haya kwa wataalamu hawa wa mawasiliano ili kufahamu mchango wao katika kusaidia utekelezaji wa maazimio ya Malabo.

“Hii inaonyesha kuwa Tanzania inazingatia na kuyachukulia umuhimu maazimio ya Malabo lakini pia CCARDESA inazingatia sana swala la usimamizi wa maarifa kwani ni sehemu ya maeneo muhimu katika mpango mkakati wake wa muda mrefu” alieleza Bi. Futh.

 Ameendelea kusema kuwa Programu ya CAADP -XP4 inaendelea kusaidia nchi za ukanda wa SADC kuweza kufikia maazimio ya Malabo hivyo mafunzo hayo ya kitaifa yana umuhimu mkubwa kwa CCARDESA kwa ujumla.

Bi. Magagula ameushukuru Umoja wa Ulaya (EU) kufadhili Programu ya CAADP -XP4 na kuwezesha kufanikishwa kwa mafunzo haya muhimu pamoja na IFAD kwa kusaidia masuala ya kitaalamu.

Nae Meneja wa Mawasiliano na menejimenti ya Maarifa kutoka Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) Dkt. Richard Kasuga amesema mafunzo haya ni moja ya mikakati ya kuhakikisha matokeo ya tafiti yanawafikia wakulima kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Kitaifa, Kikanda na kimataifa wamekuwa wakishirikiana kujenga katika masuala ya menejimenti ya maarifa na mawasiliano.

“Mafunzo haya yaliyoandaliwa kwa Tanzania ni kuhakikisha tunajenga uwezo kwa wataalamu wetu ili waweze kuchakata na kuweza kusambaza taarifa hususani matokeo ya utafiti ili yaweze kuwafikia walengwa mbalimbali wakiwemo wakulima wasindikaji na wadau wengine muhimu katika sekta hiyo” alisisitiza Dkt. Kasuga.

Ameongeza kuwa wanafanya hivyo kwakuwa kama tafiti zinazofanywa na TARI au CCADERSA unaweza kufanya vizuri na kuwainua Wananchi wa Tanzania basi unaweza pia kusaidia kuinua wananchi wa nchi nyingine za kusini mwa Afrika kama vile Malawi, Zambia, Zimbabwe na nchi zingine.

Dkt. Kasuga amesema pamoja na masuala ya kubadilishana maarifa lakini pia wana shughulika na kutangaza masuala mbalimbali kama vile utekelezaji wa maazimia ya Malabo utekezaji wake kupitia taasisi mbalimbali ili yaweze kueleweka kwa Wananchi na wadau ili wananchi waweze kushirikiana na serikali yao kuhakikisha kilimo kinawaletea maendeleo.

                                                  


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: