Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo, TARI Naliendele Dkt Fortunus Kapinga amesema kuwa ekolojia ya Mtwara inaruhusu wakulima wa Mtwara kulima mazao mengi yakiwemo mazao ya bustani, jamii ya kunde na nafaka bila kuathiri kilimo cha zao la korosho. Hivyo wanaweza kujiongezea kipato kutoka kwenye mazao hayo badala ya kutegemea zao la korosho peke yake.


Dkt Kapinga alisema kuwa mahitaji ya kiikolojia ni mojawapo ya sababu zinazotufanya tushauri zao fulani lipandwe wapi, lini na vipi".  Dkt  Kapinga ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanafunzi kutoa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo cha Kilimo Borigaram - Kigamboni walioko Kituoni hapo kwa ajili ya Mafunzo kwa vitendo (Field Practical) katika taasisi hiyo. 

Wakizungumzia tafiti za kilimo cha mboga na matunda (hotculture) wanafunzi hao wamesema wameshangaa kuona migomba ikisitawi na kuzaa  kwa wingi  na kudai kuwa wakazi wa Mtwara wanaweza kutengeneza kipato kikubwa wakati wakisubiri mavuno ya mazao mengine kama vile Korosho na Ufuta.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: