Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb)amechangia zaidi ya shilingi milioni kumi katika harambee  ya ujenzi wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Iwambi akimwakilisha Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


"Mbunge ameahidi pindi akifika Mbeya atakuja kusali Parokia ya Iwambi"alisema Mahundi


Mahundi amesema katika uongozi wake kama Mbunge atahakikisha anawafikia wanawake wote waishio Mkoani Mbeya kwa kutoa mitaji midogo midogo ili kujikwamua kiuchumi.


Aidha amewataka kushikamana kwa upendo na umoja ili kuhakikisha wanawawake wanamiliki uchumi imara ambapo kupitia Taasisi yake ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF) imetoa mchango wa shilingi milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa.


Baadhi ya viongozi wameahidi kumuunga mkono Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera aliyeahidi kuchangia shilingi laki tano,Meya wa Jiji Dour Issah Mohammed shilingi laki tano na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt Rashid Chuachua aliyeahidi kumuunga mkono kwa kuchangia shilingi laki tano.

Share To:

Post A Comment: