Baba alirudi nyumbani na kumkuta mkewe jikoni, akamkombatia, akamtazama sana mkewe na kumbusu kwenye lips, wakasalimiana na mkewe akampokea na kwenda nae chumbani kisha kurudi jikoni ili kumalizia kupika.

Ilipofika wakati wa kula, mume alikaribishwa mezani na mkewe, pamoja na watoto. Chakula kikapakuliwa na kila mmoja kuanza kula, ghafla watoto wakaguna "MMMH".

Baba anapata shauku ya kutaka kujua kilichopo ndani ya chakula, akaonja na kugundua maharage yalikuwa yameungua hivyo kutoleta radha nzuri. ..

Mama akajisikia vibaya sababu alijua kilichofanya watoto wagune, akamtizama mumewe huku akisubiria kuona kile ambacho mumewe angesema, hofu ilimjaa.

Mume akamtizama mkewe na kugundua wasiwasi alionao mkewe, akageukia sahani yake na kuanza kula, akamaliza sahani, akavuta hotpot na kuongeza chakula tena na kuweka maharage mengi zaidi ya mwanzo.

Alipomaliza akamtizama mkewe na kumuambia "Mke wangu asante kwa chakula, umenitibu njaa yangu kipenzi''.

Watoto wakamshangaa baba yao, mke akapata furaha na amani ya moyo baada ya kuona mumewe amekula na kutomkosoa kama alivyotegemea.

Baadae watoto wakamfata baba yao na kumuuliza "Kwanini ulikula chakula chote, na kumsifia japo kiliungua???".

Baba akajibu " Wanangu, niliporudi nilimtizama sana mama yenu usoni, hakuonekana yuko sawa nikagundua labda ni kutokana na uchovu wa kazi za kazini na nyumbani. Pia yeye ni binadamu, anachoka kama sisi, lakini pia nisingeweza kumkosoa kwenye hili la leo sababu hakufanya kusudi, na sio tabia yake kuunguza chakula. Tumekula chakula kitamu kilichopikwa na yeye mara ngapi??? Hivyo leo ni bahati mbaya tu na kumkosoa pale mezani mbele yenu lazima pangemfanya ajisikie vibaya, nawahusia msije kuwa-aibisha wake zenu pindi mkioa, mimi sikuwa na njaa sana ila je ningeacha kula kama mlivyo fanya, unadhani angejionaje? Hakika siku yake ingezidi kuwa mbaya."

Unachoweza jifunza kupitia story hii.
Penda kusoma mood ya mpenzi wako, kuna nyakati unaweza jikuta unatukanwa na umpendae, lakini kumbe hakupenda kukutukana bali ni hasira alizo nazo kwa wakati huo ndo zilimpelekea kumfanya hivyo. Hivyo kusomana mood ni vyema ili kuepuka migogoro.

Kosa moja lisikufanye kusahau mema 100 aliyokutendea mtu. Amini kuwa hakuna aliyekamilika, hivyo yeyote anaweza kukosea, hata wewe pia, hivyo ni vyema ukajudge mema ya mtu kabla ya kuhukumu kosa lake.
.
Tusipende kukosoa wenza wetu mbele za watu wengine hasa watoto, humfanya ajisikie aibu, vibaya, kujiona kama hana thamani. Hivyo ni vyema ukasimama nae, lakin baadae ukamuelewesha kwa utulivu zaidi na akakuelewa.

Tupende kuwatetea wapenzi wetu, tuwalinde wasiaibike, maana aibu yao ni yetu sote.

Tupende kuwahurumia wapenzi wetu, ukimuhurumia basi lazima utagundua "Ameshindwa kufanya kitu flani sababu amechoka, anaumwa" hivyo inakua rahisi kuepusha migogoro ya mara kwa mara.

Share To:

Post A Comment: