.

MKUU wa Wilaya ya Songwe Simon Simalenga amefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara yenye kipande cha urefu wa kilomita 7 kutoka Kata ya Kanga kwenda Kata ya Ifwenkenya ambayo inajengwa na Mkandarasi Elimak Engineering CO. LTD na ujenzi unaendelea vizuri.


Katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya ya Wilaya ya Songwe CPA Cecilia Kavishe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, MENEJA wa TARURA MKOA wa Songwe Kaka Kilian Haule, Meneja wa TARURA wilaya ya Songwe Eng. Yusuph Shabani, Kaimu DAS Ndugu Chesko Mbilinyi na Viongozi wengine wa Wilaya.

Akizungumza akiwa kwenye ziara hiyo Simalenga amesema kimsingi wananchi wa Wilaya ya Songwe wamejawa na moyo wa shukrani kutokana na ongezeko la fedha za Barabarabara kutoka Sh.milioni  640 walizokuwa wakipewa mpaka kufikia Sh. Bilioni 2.84 katika kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan.

Aidha amesema baada ya kazi ya ujenzi wa Mitaro unaendelea sasa, kazi itakayofuata ni kumwaga kifusi kwa urefu huo wa kilomita 7 kisha Mkandarasi atahamia Barabara ya Kata ya Galula, Chang’ombe mpaka Mbuyuni yenye urefu wa kilomita 6.

“Mpaka sasa kazi imeshafanyika kwa asilimia 25 ambapo Mkandarasi huyu anaendelea kutumia fedha zake. Ikumbukwe kwa mujibu wa Mkataba kazi hii inatakiwa kukamilika ndani ya miezi 8,"amesema Simalenga



Share To:

Post A Comment: