*************************

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa Kongole kwa Kampuni ya Multichoice Tanzania (DSTV) kwa kurusha maudhui ya kitanzania hususan Muziki na Filamu ambayo yameleta manufaa kwa wasanii.

Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Februari 3, 2022 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacqueline Woiso katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.

"Nitakutana na wasanii wote wakiwemo waigizaji na wanamuziki na kufanya nao mazungumzo, hii itatuwezesha kujua changamoto zao na mahitaji yao katika kufanya kazi zao za sanaa na hili ningeomba ushirikiano kutoka kwenu Multichoice Tanzania ili kuweza kufanikisha,"amesema Mhe. Mchengerwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo, ameahidi ushirikiano wa karibu na Wizara katika kuhakikisha sanaa inakuwa na wasanii wanapata kipato kutokana na kazi zao.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: