Ferdinand Shayo ,Arusha.


Mashindano ya Sed Miss Valentine`s 2022 yamemalizika jana huku Mrembo Jenipher Mmari akinyakua taji la Mashindano hayo na kuwashinda Warembo 14 waliokua wakiwania tajio hilo .


Jenipher Mmari alipatiwa zawadi ya Milioni 1 pamoja na zawadi nyingine nyingi ikiwemo kuwa Balozi wa Bidhaa zinazozalishwa na Kampuni ya Mati Super Brands Limited ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo.


Mrembo huyo ameeleza furaha yake baada ya kushinda taji hilo katika kinyang`anyiro kilichogubikwa na ushindani Mkali.


Mgeni rasmi katika mashindano hayo ambaye ni Katibu tawala wa Wilaya ya Babati Khalfani Matipula aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ameipongeza kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa ubunifu wa kuandaa mashindano hayo na kuyadhamini.


Khalfani amewataka warembo hao kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza utalii na fursa mbali mbali zilizoko kwenye mkoa wa Manyara.


Afisa Masoko wa Kiwanda cha   Mati Super Brands Limited Gwandumi Mpoma amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kudhamini mashindano hayo yenye lengo la kuibua vipaji vya vijana na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.


“Tumeridhishwa na uendeshaji wa mashindano haya ambayo yamezingatia misingi ya taratibu na kanuni na mshindi amepatikana kwa haki baada ya ushindano mkali” Alisema Gwandumi.

Share To:

Post A Comment: