Julieth Ngarabali. Pwani


Mkoa wa Pwani umeanzisha rasmi kituo cha pamoja cha kuhudumia wawekezaji pamoja na wafanyabishara (one stop centre) ambacho kitakua na taarifa mbalimbali za kuwezesha uwekezaji na kurahisisha utoaji huduma ndani ya muda mfupi .


Kituo hicho kina wataalamu mbalimbali kutoka taasisi zote wezeshi za Serikali zinazofanya kazi kwenye mfumo wa huduma za mahala pamoja ikiwemo mamlaka ya mapato TRA, BRELA, ARDHI ,TANESCO, TARURA, RUWASA,DAWASA, NIDA na TBS


Mkuu wa Mkoa huo Abubakar Kunenge amezindua kituo hicho Februari 14 huku na kuzisihi taasii hizo kufanya kazi kwa weledi na kasi zaidi na kushirikiana na kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kurahisisha kutoa huduma zinazotakiwa na wawekezaji katika kufanikisha uwekezaji mkoani humo


"Kwa kufungua hiki kituo ambacho kina taarifa mbalimbali za kuwezesha kuonyesha mazingira ya biashara ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano Samia Suluhu ambalo vile vile lilisisitizwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba tufungue vituo kama hivi "amesema Kunenge na kuongeza


" tena kituo  kipo jirani kabisa na ofisi yangu mlango wa pili tu kwa hiyo wadau wetu watakapokuja apa wataweza kutatuliwa changamoto zao hapa hapa nilipo na mimi kwa maana hiyo hiki ni kituo ambacho ninakisimamia mwenyewe"


Naye Katibu Tawala wa mkoa huo Mwanasha Tumbo amesema jambo kubwa walilogundua ni wawekezaji wengi wanaokuja kuwekeza wakishapita kituo cha uwekezaji TIC na EPZA wanaenda moja kwa moja katika maeneo ya ujenzi wa viwanda na  biashara huku mkoa  na Wilaya ukiwa hauna taarifa za ujio wao hadi wanapopata shida .


Awali kabla ya uzinduzi huo viongozi mbalimbali kutoka sekta binafsi walikutana na uongozi wa mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine ya kimkakati  walieleza changamoto  zao na kwa pamoja wakakubalian kuzitatua ili kwa pamoja waweze kuinua uchumi

Share To:

Post A Comment: