Mwandishi wetu,Arusha


Zaidi ya kiasi cha sh,1.5 bilioni zimeokolewa katika ujenzi wa jengo la Ufundi Tower linalojengwa katika chuo cha ufundi mkoani Arusha (ATC) ambalo awali serikali ilivunja mkataba wa ujenzi na mkandarasi wa awali.


Awali chuo hicho kiliingia mkataba na kampuni ya Tanchi Brothers  kujenga jengo hilo kwa kiasi cha sh,6.8 bilioni ambapo tayari jumla ya sh,3 bilioni alishalipwa kupitia mfumo wa malipo wa force account.


Ujenzi wa jengo hilo ulikuwa ukifadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (Afdb) lakini serikali kupitia wizara ya fedha iliufuta mkataba huo kutokana na kuibuka kwa utata wa gharama za ujenzi.


Akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo waziri wa elimu,sayansi na Teknolojia nchini,Prof Adolf Mkenda alisema kwamba serikali serikali iliamua kufuta mkataba wa awali wa ujenzi wa jengo hilo Desemba 2019 wa sh,6.8 bilioni kwa kuwa haukuwa na maslahi.


"Mkataba haukuwa mzuri sana wizara ya fedha ikaamua kuusimamisha kuliibuka utata wa gharama za ujenzi hapo awali" alisema Prof Mkenda


Hatahivyo,alidai kwamba Mara baada ya kufuta mkataba huo serikali iliamua kuwatumia wakandarasi wa chuoni hapo ambapo kwa sasa unagharimu sh,5.5 bilioni na umefanya kuokoa kiasi cha zaidi ya  sh,1.5 bilioni.


Naye mkandarasi anayesimamia ujenzi wa jengo hilo,Injinia Faraj Magania  alisisitiza kuwa kwa sasa ujenzi wa jengo hilo unafadhiliwa na fedha za Uviko-19 na unataraji kukamilika mwezi Mei ambapo umekamilika kwa asilimia 60.

Share To:

Post A Comment: