Serikali kupitia fedha za uviko 19 imefanikiwa kutokomeza  maadui watatu ikiwemo maradhi,elimu na umaskini katika halmashauri ya Meru iliyopo mkoani Arusha.

Akizungumza katika ziara ya kamati ya siasa ya  mkoa wa Arusha ya kaguzi ya miradi ya maendeleo kupitia fedha za uviko 19 wa ujenzi wa madarasa pamoja na vituo vya afya katika halmashuri hiyo,Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Arusha Zelote Stevene alisema wametokomeza maadui hao kupitia mradi wa ujenzi wa madarasa na vituo vya afya kupitia fedha hizo.

"Ni faraja kubwa sana serikali kutoa fedha takribani sh.tirioni 1.3 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule na vituo vya afya  ikiwa halmashauri ya meru ilitolewa takribani sh.bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,"alisema Mwenyekiti Zelote.

Naye Katibu wa CCM mkoa wa Arusha,Mussa Matoroka alisema pamoja na ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa hayo kwa asilimia 100 ni vyema viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo wakaendelea kuwaelimisha na kuwafahamisha wananchi juu ya utekelezaji wa miradi ya serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashuri ya Meru,Jeremia Kishili alisema anaishukuru serikali kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi  wa madarasa kwani imewaondolea adha ya kuchangishana na wananchi kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule hali iliyokuwa inasababisha wanafunzi waliochagulia kuanza masomo kwa awamu.

"Sasa hivi tungekuwa tunaanza kukimbizana na wananchi katika kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa lakini sasa hivi hali yao shwari hivyo wanachotakiwa ni kuwaandaa watoto tayari kwa kuanza shule na ninawahimiza wazazi kuwa kipindi hiki hatuna awamu mbili kama ilivyozoeleka,"alisema Kishili

Aidha aliongeza kuwa nivyema wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza takribani 6707 wakaanza masomo kwa muda uliopangwa na serikali.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru,Mwalimu Zainabu Makwinya alisema kwa upande wa tozo pia walipata fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa mawili katika shule ya sekondari King'ori ambapo yamekamilika kwa asilimia 100.

"Sasa hivi sitakuwa na kukimbizana na wazazi kwa ajili ya michango  kwa lengo la kumpeleka mtoto shule hivyo na wahimiza walezi na wazazi kuwa kuanzia januari 17 majira ya jioni tutapokea taarifa ya watoto walioripoti shuleni na ambao hawatafanya hivyo tutawachukulia hatua kupitia watendaji wa mitaa yao,"alisema Mkurugenzi Makwinya.
Nao baadhi ya wananchi wa halmashuri ya Meru walisema walikuwa wanapata changamoto ya kuchangishana kidogo kidogo kupitia kila nyumba kwa ajili ya ujenzi wa madarasa lakini sasa hivi serikali imewarahisishia kazi yao ni kuwapeleka watoto shuleni.

Share To:

Post A Comment: