Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Christina Musyani akizungumza leo Mkoani Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Christina Musyani akionesha baadhi ya silaha ambayo wamezikamata.


JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa za kujihusisha na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Katika taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Christina Musyani iliyotolewa leo Januari 18, 2022 imewataja watuhumiwa hao kuwa ni MSAFIRI PETER MWAHONJE [46] Mkazi wa Usangu Wilaya ya Mbarali, BONIFACE HARISON SHUPA [36] Mkazi wa Matundasi Wilaya ya Chunya na ONESMO BOLISI MWACHAWI [38] Mkazi wa Makongolosi Wilaya ya Chunya.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Watuhumiwa walikamatwa mnamo Januari 15, 2022 majira ya saa 23:45 usiku huko Mji Mdogo wa Makongolosi, Wilaya ya Chunya katika misako inayoendeshwa na Jeshi la Polisi dhidi ya wahalifu wa matukio mbalimbali. 


Katika upekuzi uliofanywa kwa watuhumiwa, walikutwa na silaha bunduki mbili Bastola moja na Gobore moja zilizotengenezwa kienyeji, risasi 10 za Shot Gun, simu za mkononi tatu, tochi moja, panga moja, kofia mbili na mizula miwili ambavyo hutumia katika matukio ya uhalifu.


imeeleza kuwa Watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kuhusika kwenye matukio mawili ya unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo tukio la tarehe 02/01/2022 majira ya saa 21:30 usiku huko matundasi ambapo walivamia dukani kwa ANDREAS JOHN [22] Mfanyabiashara na Mkazi wa Matondo na kumpora fedha taslimu Tshs.1,100,000/= pamoja na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Tshs.5,490,000/= na kumjeruhi mke wa mhanga aitwaye SARAH FRANK [21] Mkazi wa Matondo. Pia mnamo tarehe 14.01.2022 majira ya saa 20:00 usiku walivamia dukani huko eneo la Mnazi Mmoja Chunya na kupora fedha taslimu Tshs.1,925,000/=, simu za mkononi na vitu mbalimbali. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani. 

Share To:

Post A Comment: