Waziri Bashungwa amesema uchambuzi wa taarifa kuhusu ufanisi wa Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, unaonyesha kuwa Halmashauri 113 zimekusanya kwa asilimia 50 au zaidi ya lengo la mwaka, na Halmashauri 71 zimekusanya chini ya asilimia 50. 


Alisema ulinganisho wa ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani unaonyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imeongoza katika Halmashauri zote 184 kwa kukusanya asilimia 102 ya makisio yake ya mwaka, ikifuatiwa na Halmashauri za Wilaya ya Kaliua, Shinyanga na Mlele ambazo zimekusanya kwa asilimia 91, ya lengo la mwaka.


" Hata hivyo, kuna uwezekano wa Halmashauri hizi kuwa na makisio yasiyoakisi uhalisia wa uwezo wake wa ukusanyaji mapato ya ndani hivyo kuhitaji kufanya mapitio ya bajeti ili kuongeza bajeti ya makusanyo na kuweza kuendelea kufanya matumizi ya fedha kutoka kwenye makusanyo hayo." 


Aidha, Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli na Kilindi zimekuwa za mwisho kwa kukusanya asilimia 27 ikifuatiwa na Halmashauri Wilaya ya Bunda ambayo imekusanya asilimia 28.

Share To:

Post A Comment: