Na,Jusline Marco:ArushaNaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Tulia  Ackson ametunuku vyeti wahitimu 2481 wa shahada ya Uzamili,Stashahada,Astashahada  pamoja na Shahada katika nyanja mbalimbali kwenye maafali ya 23 ya Chuo cha Uhasibu Arusha.


Akitunuku vyeti hivyo katika hafla iliyofanyika jijini Arusha Mhe.Tulia ameipongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kuongeza kozi katika ngazi zote na uwekaji wa mitaala mahiri ambayo inatumika kutoa kozi hizo katika kuwaandaa wataalamu kujifunza kwa vitendo zaidi na kuwaongezea thamani katika ushindani wa soko la ajira.


Aidha amesema pamoja na kuwaandaa wataalam,tafiti zinazofanywa na chuo hicho za kuleta mchango chanya katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya rasilimali watu,mazingira wezeshi ya biashara,masoko, utaratibu na mapinduzi 

Ya kidigitali huku dhamira ya tafiti hizo kufikia lengo la muda mrefu la mpango wa tatu ni kuiwezesha Tanzania kufikia nchi ya uchumi wa kipato cha kati na yenye kiwango cha juu cha maendeleo ya watu.


Mhe.Tulia amewataka wahitimu hao kutafakari namna ambavyo watatumia elimu waliyoipata kupambana na umaskini kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja,jamii inayomzunguka* na Taifa kwa ujumla ili kuweza kuisaidia jamii katika kuleta maendeleo.


"Serikali imeandaa dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 itakayoongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii ili kuamsha,kuungalisha na kuelekeza juhudi na fikra zetu na rasilimali za taifa letu yatakayotuwezesha kufikia malengo yetu na kustahimili ushindani wa kiuchumi kitaifa na kimataifa.


Ameongeza kwa kuwataka wahitimu hao kufahamu kuwa elimu siyo zana ya maandalizi ya maisha bali wafahamu  kuwa elimu ni maisha yenyewe na ni mwanga wa maisha katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiuchumi kijamii kisiasa na kiutamaduni.


Naye Prof.Eliamani Sedoyeka katika maafali hayo amesema chuo hicho mpaka sasa kinatoa kozi 17 ngazi ya Astashahada,kozi 17 ngazi ya Stashahada,kozi 18 ngazi ya Shahada na kozi 12 ngazi ya Shahada ya uzamili ambapo mwaka 2022 chuo kinatarajia kutoa Shahada ya Uzamivu kwa ushirikiano wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha  Nelson Mandela kwa kuanzisha kozi maalum za kitaalam ikiwemo kozi ya ACCA,CPA,CPB na ICDL.


Prof.Sedoyeka ameongeza kuwa matarajio ya chuo hicho ni kuhakikisha wataalam watakaokidhi vigezo na matakwa ya soko la ajira kitaifa na kimataaifa kupitia mitaala ambayo wanafunzi watajifunza kwa vitendo kuliko nadharia.


"Pamoja na mfumo huo tumeanzisha mfumo wa uanagenzi ambao unawawezesha wanafunzi kusoma kwa vitendo zaidi katika maeneo ya kazi wakati wanasoma,mfumo huo tunautekeleza kwa ushirikiano na wadau mbalimbali."alisema Prof.Sedoyeka


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho Dkt.Mwamini Tulli amesema ongezeko la kozi katika chuo hicho ni mchango wao katika kuiwezesha Tanzania kutimiza malengo ya maendeleo endelevi ya mwaka 2016 hadi 2030 sambamba na utoaji wa elimu bora.


"Kuanzisha kozi mbalimbali zinazoendana na mahitaji ya soko la sasa nchini ni moja ya mikakati ys chuo ambapo chuo kinaendelea kufanya tafiti mbalimbali kujua mahitaji ya watanzania na kianzisha kozi mbalimbali zinazokidhi mahitaji na kuondoa adha ya watanzania kutafuta kozi hizo nje ya nchi kwa gharama kubwa.


Vilevile ameahidi kushirikisna na kifanya kazi na uongozi wa chuo hicho kuhakikisha mikakati waliyojiwekea ya utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa mafunzo,kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam inatekelezwa ili kulinda hadhi iliyopo.

Share To:

Post A Comment: