***************

Na. John Mapepele

Timu ya Ghana wameibuka mabingwa kwenye mashindano ya soka barani Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021) baada ya kushinda Liberia magoli 3-2.

Mchezo wa fainali hiyo umechezwa leo Disemba 4, 2021 kwenye uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul akiwa na Katibu Mkuu, Dk. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi ameongoza watanzania na wadau wa mchezo huo kutoka mataifa mbalimbali kushuhudia mchezo huo.

Kufuatia ushindi huu Ghana inakuwa bingwa wa mashindano ya CANAF 2021 ikifuatiwa na Liberia, Angola inakuwa mshindi wa tatu na Tanzania wenyeji wanakuwa wa washindi wa nne.

Timu zote nne ambazo ni washindi zinakuwa zimefuzu kuwakilisha Bara la Afrika kwenye mashindano ya mchezo huo katika mashindano ya dunia nchini Uturuki Oktoba 2022.

Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka kwa wenye ulemavu (WAF) Mateus Wildack ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi mahiri wa kuiletea Tanzania maendeleo na kuwashirikisha walemavu katika michezo.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: