Na Woinde Shizza , Arusha 



Benki ya CRDB Kwa kushirikiana na shirika la ndege Tanzania (ATCL) leo limeingia mkataba wa makubaliano ya  ulipaji wa tiketi za ndege kupitia huduma za Benki hiyo  ikiwemo Simu banking ,mawakala wake waliotapakaa kila wilaya ,matawi yao yote ya Benki pamoja na Simu ya kawaida ya mkononi.



Akiongea wakati wa kuingia mkataba huo  mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela alisema kuwa wameamua kuingia mkataba huo  ili kuweza kuendelea kuwarahisishia wateja wao upatikanaji  wa huduma Kwa njia ya haraka.


Alisema kuwa huduma hii itasaidia kuweza kuwarahisishia wateja wao kukata tiketi kupitia mfumo wa kidigitali kwani watakata tiketi kwa kupitia simu zao za mikononi ikiwemo simu za Android pamoja na  simu za kawaida ,pamoja na mawakala wao wote waliopo hapa nchini nia.


"Ushirikiano huu pia unaangalia  sisi Kama nchi tunafanya nini ,pia tunataka tuangalie namna gani tunawapunguzia wananchi wetu gharama badala ya mwananchi kuangaika kuwasha gari yake kwenda kukata tiketi au kuchukuwa bajaji kwenda kukata tiketi aweze kutumia simu yake kupata huduma hiyo "alisema Nsekela 


 Mpaka sasa benki ya CRDB imejiongeza na inamatawi nje ya nchi   ikiwemo Lugumbashi nchini Kongo na wapo kwenye hatua za mwisho za kufungua tawi nchini kenya


Alibainisha kuwa wamekuwa wanautaratibu wa kusikiliza maoni ya wateja na wazo hili walipata kutoka Kwa wateja na ndio maana wakaamua kulifanyia kazi .


Kwa upande wake mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) Muhandisi Ladislaus Matindi alisema kuwa  wameungana ili kuweza kumsaidia mteja kufaidi kupitia teknolojia ndio maana wamejiunga na benki hii ili wamrithishe mteja huku akifafanua kuwa ukitaka mteja akuamini lazima umpe  huduma bora.


"Ushirikiano huu ni wamwanzo na utakuwa endelevu ili kuweza kufikia watanzania wengi zaidi ,nanapenda nishukuru Serikali Kwa kuendelea kutuamini na kuendelea kiwekeza ndani ya shirika letu la ndege pamoja na watanzania kuendelea kutuamini na kuendelea kutumia shirika letu"alibainisha Matindi 


Alisema kuwa adi sasa ATCL inatoa huduma katika vituo 15 ndani ya nchi na Kwa upande wa nchi zaidi ya nchi 11 wanapeleka ndege zao  na wanampango pia wakuongeza wigo zaidi   wa kupeleka safari zao  katika nchi  nyingine ikiwemo  Nchini Johanesburg  nchini Afrika kusini,Kinshasa,pamoja na Lagos -Nigeria

Share To:

Post A Comment: