Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ambaye juzi ijumaa alihukumiwa miaka 30 gerezani, kesho
Jumatatu tarehe 18 Oktoba 2021, atarejea tena Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha kuendelea kusikiliza kesi nyingine inayomkabili ya Uhujumu Uchumi.
Sabaya mwenye miaka 34 na
wenzake sita, wanakabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi katika
Mahakama hiyo ambayo Ijumaa iliyopita ya tarehe 15 Oktoba 2021,
ilimhukumu kifungo hicho jela yeye pamoja na wenzake watatu.
Wakati akiendelea kutumikia
adhabu hiyo, kesho Jumatatu, atarejea tena mahakama hapo kuanza
kusikilizwa mfululizo kwa kesi nyingine ya uhujumu uchumi inayosikilizwa
na Hakimu Mkazi Patricia Kisinda.
Kesi
hiyo ya uhujumu uchumi inamashtaka mbalimbali ikiwemo kuongoza genge la
uhalifu pamoja na utakatishaji fedha inayomkabili Sabaya na wenzake
sita ambao ni, John Aweyo, Watson Mwahomange, Enock Mnkeni, Sylvester
Nyegu, Nathan Msuya na Jackson Macha.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wote wanatuhumiwa kujipatia Sh.90 milioni kutoka kwa
mfanyabiashara Fransis Mrosso kinyume na sheria.
Post A Comment: