MKUU
wa mkoa wa Arusha, John Mongella, amezitaka halmashauri zote za
wilayani katika Mkoa huo kuhakikisha zinakuwa na Waratibu wa
Tasaf,waadilifu ambao watahakikisha wananchi wenye hali duniza maishaI
wanaboresha maisha yao vinginevyo hatasita kuwaondoa kwenye nafasi hizo
kwa kuwa watakuwa wanakwamisha lengo zima la kuwezesha wananchi kupata
maisha.
Rc Mongela,ameyasema
hayo leo alipokuwa akifungua mafunzo ya awamu ya pili sehemu ya tatu ya
mpango wa TASAF,yanayowashirikisha mdiiwani,wabunge ,Waratibu wa Tasaf
jiji,pamoja na. watendaji wa halmashauri ya Jiji la
Arusha,yanayofanyika ukumbi wa Katibu tawala wa mkoa.
Rc Mongella,amesema mkoa utasimamia Tasaf,ili iweze kutekeleza lengo lake la.kuwawezesha wananchi wenye hali duni ya maisha na kiuchumi ili waweze kuboresha maisha yao hivyo lazima wawepo waratibu wenye sifa ,ubunifu na uwezo wa kufanya kazi zitakazosaidia kaya masikini kuinuka kiuchumi.
Amesema Tasaf inafanya kazi kubwa ya kuboresha maisha ya wananchi wenye hali duni ili nao wawe na maisha bora, kupitia Tasaf wapo wananchi walookuwa na hali duni tangia ianzishwe miaka 7,leo wanaboresha maisha ambapi wameweza kuanzisha shughuli za kiuchumi na sasa wana maisha mazuri
Ameonya mapungufu yaliyojitokeza kwenye utekelezaji wa Tasaf awamu ya kwanza na. ya Pili ya Kiungiza kaya ziisizokuwa na. sifa yasijirudie na akawataka madiwani wahakikishe wanasimamia zoezi hilo la utambuzi wa kaya duni kuhakikisha kaya zitakazoingjzwa kwenye mpango huo wawe ni walengwa ambao ndio wenye uhifaji na si vinginevyo.
Akitoa
nasaha zake mkuu wa wilaya ya Arusha Sophia Mjema,amesema mafunzo hayo
yanawajengea uelewa madiwani na Waratibu ili waweze kushiriki
kaikamilifu katika utekelezaji na usimamizi wa mpango huo wa Tasaf,ili
kuepuka Wasio na.sifa wasiingizwe kwenye mpango huo Bali wananchi wenye
hali duni
ndiio waweze kuingizwa kwenye mpango huo hatimae waboresha maisha yao.
Amewaambia
madiwani hao kuhakikisha kuwa wanazitambua kaya zote zenye hali duni
ili kuwezesha wahitaji kupata ruzuku ya fedha inayotolewa na Tasaf,
waweze kunufaika kwa kuwa wanazifahamu kaya duni zenye uhitaji ziweze
kunufaika n.a. hatimae ziboreshe maisha.
Amesema
yeye atashiriki zoezi hilo ili kuondoa udanganyifu wa kwa kuingiza
wasiokuwa na sifa,na hataki wilaya yake kuwepo na wahitaji hewa bali
kuwepo na idadi halisi ya wahitaji halisi na akaonya kwamba yeyote
akaefanya udanganyifu kwa kuweka kaya hewa huyo atadhughulikuwa kwa
majibu wa sheria.
Mbunge
wa jambo la Arusha, Mrisho Gambo,amesema wapo wasiokuw na. sifa
wanafanya kazi Tasaf na. matokeo yake ni kukosekana kwa,ufanisi
Ameitaka
Tasaf kuwakumbuka wazee kwa kutambua kuwa wazee wameifanyia mambo mengi
nchi hii lakini wamekuwa wakisahaulika kwenye miradi mbalimbali ya
kuboresha maisha wakati changamoyo ya umasikini haina umri.
Tasaf,umekuwa
ni msaada mkubwa kwa wananchi hivyo akamuomba mkuu wa mkoa kuweka jicho
la zida kwenye miradi na ushauri serikali iipitie na. kuratibu ipasavyo
ili kuonfoa udanganyifu unaweza kujitokeza na kuingizwa kaya hewa.
Kwa
upande wake Mstahiki meya wa Jiji la Arusha, Maxilian Illanghe,amesema
katika salamu zake kwamba madiwani wanasimamia Programu hiyo ya
Tasaf,ipasavyo,kwa kuhakikusha vigezo vilivyo wekwa vya walengwa
kuingizwa kwenye programu hiyo ni wale wenye uhitaji na hakuna endeleo.
Amesema mafunzo hayo yatawawesha madiwani kusimamia ukusanyaji mapato ambayo yatasaidia wajasriamali katika kipindi cho na hivyo kupunguza maskini katika jamii.
Awali
mwakilushi wa mkurugenzi miuu wa Tasaf, Janeth Madulu, alisema kuwa
mara baada ya mafunzo hayo wataenda mitaani kwa ajilivya utekelezaji wa
zoezi hilo la kutambua kaya duni ili ziingixwe kwenye mpango huo.
Ameongeza
kwamba asilimia 12% ya Kaya umaskini umepungua ambapo kupitia
Tasaf,walengwa wameweza kufanya shughuli za ujasiria mali
Post A Comment: