Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngorongoro Girls.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha wakikagua ujenzi wa Jengo la Maabara.

Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Arusha akizungumza na Wananchi wa kata ya Enduleni wilayani Ngorongoro.

Na Imma Msumba,Loliondo

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen ameridhishwa na ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Ngorongoro Girls iliyopo kata ya Enduleni Wilayani Ngorongoro yenye wanafunzi 280 na walimu 12 wa kidato cha kwanza na pili.

Haya yamejiri wakati wa ziara yake ya kukagua uhai wa chama Mapinduzi katika ngazi ya mashina na matawi sambamba na utekelezaji wa ilani ya Chama cha mapinduzi na kukagua shule hiyo yenye majengo saba yaliyogharimu Bilioni 2.3 fedha ambazo ni miradi inayotelelezwa kwa Mpango wa lipa kutokana na Matokeo (EP4R).

Zelothe amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala kwa usimamizi mzuri wa shule hiyo na kwa ubunifu na utendaji kazi wenye tija katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa,mabweni,na nyumba za walimu na utekelezaji wa fedha za P4R.

Naye Diwani wa kata hiyo ya Enduleni Emmanuel Shangai ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Chama cha Mapinduzi kwa kuongeza thamani ya Jimbo la Ngorongoro kwa ujenzi wa shule hiyo ya wasichana.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti Zelothe alikagua pia ujenzi wa maabara inayojengwa kwa kupitia fedha za Programu ya EP4R, na kuhaidi kupitia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kuwapatia fedha kiasi cha Milioni mbili kwa ajili ya ununuzi wa viti vya wanafunzi katika shule hiyo.

Share To:

Post A Comment: