Teddy Kilanga


Katibu Mkuu wa wizara ya fedha na Mipango ,Emmanuel Tutuba amehimiza taasisi mbalimbali kuwa wahadilifu katika kusimamia sheria na taratibu ,kanuni na miongozo ya usimamizi wa ununuzi wa umma ili bidhaa zinazonunuliwa ziwe katika bei inayowiana katika soko.


Akizungumza katika kikao cha bodi ya mamlaka ya udhibiti wa usimamizi wa ununuzi wa umma(PPRA) kilichofanyika jijini Arusha,Tutuba amesema huduma zinazonunuliwa katika masoko zileta unafuu katika ununuzi  na miradi inayotekelezwa iwe na gharama ndogo na kuwa mstari wa mbele kusimamia uadilifu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mtu anayepata zabuni apate kwa haki.


Aidha Katibu Tutuba amesema  mtu anayepata zabuni asiwe kwa kupendelewa au kutoa rushwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanatoa fursa sawa kwa wafanyabiashara wote ili wafanye biashara zao kwa uwazi na haki.


Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo amesema wataendelea na juhudi na kufanya kazi kwa bidii pamoja na udhibiti wa ununuzi wa umma kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: