WAZIRI wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula akijibu maswali ya wabunge Bungeni Jijini Dodoma
Mbunge
wa Viti Maalumu kupitia NGOs Neema Lugangira akitoa Mchango wake kwenye
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje
WAZIRI wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula amesema
kabla ya mwaka huu kuisha Sera ya Nje inayojumuisha Sera ya Diaspora
itakuwa tayari na hiyo ni kwa kutambua uhimu wa diaspora katika
kuchangia maendeleo na masuala ya diaspora yanapewa kipaumbele.
Ameyasema
hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu kuhusu Ushauri aliotoa Mbunge
wa Viti Maalumu kupitia NGOs Neema Lugangira katika Mchango wake kwenye
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje alipoitaka Serikali itunge Sera ya
Diaspora ambayi ni Sera hiyo ni muhimu na kwa sababu jambo hilo haliwezi
kuendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje pekee kwa sababu linahusu Sekta
nyingi.
“Mh
Spika ningependa kugusia suala la diaspora hili jambo lilishawai
kujadiliwa sana na tulishapiga hatua ambapo diaspora hao mikutano
mbalimbali ilifanyika nje ya nchi na walishiriki hata kutoa maoni kwenye
katiba mpya ambayo inapendekezwa sasa nimefurahi kwenye Hotuba, Mhe
Waziri amewagusia suala la diaspora na hata kwenye mapendezo ya kamati
nao wameguaisia suala la diaspora" Alisema
Mbunge
Lugangira aliendelea kusema kwamba lile zoezi la ziara nyingi nje ya
nchi zilizokusanya maoni ya diaspora na hadi kuwashirikisha diaspora
kwenye huo mchakato Katiba mpya inayopendekezwa yalipelekea hayo
kuanzishwa kwa Idara ya Diaspora ndani ya Wizara na Mambo ya Nje ambapo
kulikuwa na Mkurugenzi kwenye jukumu la kufanya coordination na
ufuatiliaji.
Aliendelea
kusema kwamba hivi sasa imeonekana kama jambo hilo limerudi nyuma kwa
sababu hivi sasa kuna Sheria ambazo zinamzuia Mtanzania anayeishi Nje ya
Nchi kumiliki ardhi lakini pia zipo Sheria ambazo zinamnyima haki ya
kurithi mali za wazazi wake kwa sababu Sheria zimeweka hicho kizuizi na
kwa msingi huo anapendekeza Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi iandae Sera
ya Diaspora.
Alisema kwa
sababu nchi nyengine wanatumia diaspora kuendeleza uchumi na uwekezaji
hivyo Serikali itunge Sera ya Diaspora na Sera hiyo ni muhimu kwa sababu
nasi pia Tanzania tutaweza kutumia diaspora kuchangia kukuza uchumi wa
nchi yetu ambayo ni nchi yao pia.
“Mh
Spika Mbunge mwenzangu ametoa mfano wa India lakini naomba nilitolee
ufafanuzi. Nchini India walichofanya wamewapa Wahindi wanaoishi Nje ya
India kitu kinachoitwa Pasipoti ya People's of India Origin (PIO) ambayo
PIO hiyo inamruhusu mwenye pasipoti ya PIO kuingia India na kutoka muda
wowote bila Viza, in mruhusu kuwekeza kwenye hiyo nchi na kufanya kazi
kwenye Sekta zote kasoro Sekta ya Ulinzi na Usalama” Alisema Mbunge
Neema Lugangira
Alisema
pia "Jambo lingine ambao Wahindi wenye Pasipoti ya PIO ambalo hawatakiwi
kufanya ni kujishughulisha na masuala ya kisiasa na kupiga kura hivyo
mantiki hiyo Mhe Spika napendekeza na sisi kama Tanzania tufike huko na
hatuwezi kwenda huko bila kuwa na Sera ya Diapsora na Sheria ambayo
itaelekeza ni namna gani tutatoa fursa kwa diaspora.
“Katika
jambo hili naomba tusichanganye mambo mawili ya diaspora na uraia pacha
hilo la uraia pacha tumelijadili na limeoneka lina ugumu hivyo
lisituchukulie muda lakini la diaspora lipo ndani ya uwezo wetu na hata
sasa hivi diaspora wananunua viwanja wanawekeza na wanafanya hivyo
kutumia kwa kutumia njia zisizo rasmi kwa kutumia ndugu jamaa na
marafiki “Alisisitiza Mbunge Neema Lugangira
Alisema
hivyo wanachotakiwa kufanya ni Wizara ya Mambo ya Nje iwe na Sera ya
Diaspora ili kuweka suala hilo rasmi na kupitia Sera hiyo Nchi itaweza
kujua kuna diaspora wangapi na mchango wao katika ukuaji wa uchumi ni
upi.
“Kwa kumalizia
naomba Mhe Waziri atapokuja kuhitimisha atuambie na atupe Msimamo wa
Serikali wa kuja na Sera ya Diaspora ambayo itawezesha Watanzania
wanaoishi Nje ya Nchi kuchangia kwenye maendeleo ya nchi na kutoa
rasimali fedha amboyo tunaihitaji kwenye uwekezaji ”Alisema Mbunge Neema
Awali
wakati anaanza Mchango wake Mbunge Neema Lugangira alisema "Nampongeza
sana Mhe Rais Samia Suluhu kwa ziara aliyoifanya nchini Kenya ambayo
imeleta matokeo makubwa sana katika diplomasia ya uchumi inayohitajika
nchini na kama unavyofahamu wiki hii Kenya na Tanzania wamekubaliana
kuondoa Tozi za biashara 30 na kuna mchakato wa kuondoka Tozo 34 na hayo
ni matokeo ya jitihada kubwa za Mhe Rais lakini pia nimpongeze Mhe
Waziri wa Viwanda na Baishara kwa kufanikisha jambo hilo".
Mbunge
Neema Lugangira alisisitiza kwamba Mtazamo wa Mhe Rais Samia Suluhu
Hassan kuhusu Kenya kwamba sio adui wetu uungwe mkono kwani Kenya ni
mshindani mwenzetu, wanatupa changamoto, tusiwaogope kutokana na kwamba
tunaweza kushindana nao na kuwakabili.
“Niungane
na Wabunge wenzangu ambao wametoa pongeza kwa Mhe Rais Samia Suluhu
Hassan kuhusu kutengeneza safu mpya kwenye Wizara ya Mambo ya Nje
iliyojaa wabobezi kwenye fani ya diplomasia ikiongozwa na Waziri Balozi
mwanamama Liberata Mulamula, Naibu Waziri Mbaruku, Katibu Mkuu Balozi
Sokoine, Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Rajabu na Chief Protocol Balozi
Mndolwa ambao tunaimani nao kubwa sana na sasa tunaona diplomasia
nchini inapaa” Alisema Mbunge Lugangira
Post A Comment: