"Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameliteka basi la abiria lenye namba za usajili T 116 BHD mali ya kampuni ya Scorpion lililokuwa likitokea mkoani Shinyanga kuelekea Kasulu mkoani Kigoma na kisha kuwapora vitu mbalimbali abiria waliokuwa wakisafiri katika basi hilo."

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo akiwa katika Kituo kidogo cha Polisi cha Makere Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi James Manyama amesema tukio hilo limetokea katika Pori la lililopo jirani na kambi ya wakimbizi ya Nduta.

Aidha katika tukio jingine Kamanda Manyama amesema Jeshi hilo limeendelea Operesheni Maalum na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa mbalimbali pamoja na magunia 18 ya bangi yaliyokuwa yakitarajiwa kusafirishwa kuelekea nchi ya jirani ya Burundi.Source : ItvShare To:

Post A Comment: