WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amezielekeza Mamlaka za Majisafi na usafi wa Mazingira zote nchini kwa tamko rasmi kuanza kutekeleza ufungaji wa Pre-paid meter yaani (MITA YA MALIPO KABLA) ambayo itasaidia kuondoa malalamiko makubwa kwa wananchi kuhusu ankara za maji " Water Bill". 

Waziri Aweso amesema Wizara kupitia Mamlaka za Maji zoezi lianze mara moja kwa Kufunga Pre-paid meter kwa hatua za awali kwa Watumia Maji Wakubwa wote (Taasisi za Umma, Binafsi na Viwanda) pamoja na ofisi mbalimbali,akisisitiza sasa rasmi utaratibu huu uanze na unaenda kuwa muarobaini wa changamoto hii ya muda mrefu.

Pamoja na hao ameelekeza Viongozi wote sasa waanze kama mfano kufungiwa mita hizo za maji  na hatua kwa hatua kwa awamu iwafikie wananchi wote.

Aidha, Mh.Aweso ametembelea na kukagua Mtambo wa Kupima Dira za Maji "Meter Testing Bench"
Akiwa hapo ameagiza wakati mabadiliko yanaendelea kuelekea mfumo wa Pre-Paid Meter zoezi la kuendelea kutumia mitambo hii kupima ubora wa mita za wananchi liendelee wakisubiri kufikiwa na mfumo mpya na kuiagiza Mamlaka ya Maji Arusha kufanya zoezi hili mtaa kwa mtaa watu wahakiki ubora wa mita zao.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: