MBUNGE wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga (CCM) Dunstan
Kitandula ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha kusahaulika kwa
barabara ya Mabokweni - Maramba, Mtoni Bombo hadi Korogwe kwenye
makutano ya Umba mpaka Same wilayani Kilimanjaro ambayo amekuwa
akiizungumzia kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo bungeni.
Amesema
barabara hiyo ilikwisha kuahidiwa na Marais watatu ambao ni Hayati
Benjamini Mkapa,Jakaya Kikwete na hayati Dkt John Magufuli lakini kwa
kushangaza haipo hata kwenye upembuzi yakinifu jambo ambalo
linamsikitisha kutokana na namna alivyoipigania kila wakati bila
mafanikio.
Kitandula
aliyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hoja wakati wa
Bajeti ya Wizara ya Ujenzi ambapo alianza kwa kukishukuru Chama cha
Mapinduzi (CCM) kwa mara ya kwanza kutambua umuhimu wa Barabara ya
Maramba –Mabokweni Mtoni Bombo kuelekea Korogwe na makutano ya Umba
mpaka Same na kuiingiza kwenye ilani ya CCM ya Uchaguzi.
Mbunge
Kitandula alisema lakini licha ya kuingia kwenye ilani kwa masikitiko
makubwa bajeti hiyo imeisahau barabara hiyo ambayo aliizungumzia miaka
10 mfululizo huku wakipewa ahaidi kwa vipindi tofauti kwamba itajengwa
kwa kupitia MCC kipindi fulani mpango ambao uliyeyuka; na kwa wakati
mwengine aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akahaidi
kwamba barabara hiyo itaingizwa kwenye mpango wa usanifu lakini mpaka
leo haitajatokea.
“Lakini
pia Barabara hii ilihaidiwa na Marais Watatu Benjamini Mkapa,Jakaya
Kikwete na John Magufuli lakini cha kushangaza haipo hata kwenye
upembuzi yakinifu"
"Barabara hii kwa nyakati tofauti imezungumziwa
vilevile na Shehe Mkuu wa Tanzania Mufti Shehe Abubakari Zuberi ambaye
alipewa ahaidi na Rais Hayati John Magufuli pale Korogwe na
haijatokea…halikadhalika Askofu Mkuu wa Angalikana aliizungumzia
barabara hii naye akaahidiwa itajengwa na haijajengwa. Akionesha
msisitizo Kitandula akahoji kama mmepuuza maneno ya Kitandula hata hawa
viongozi nao mnayapuuza, hivi muambiwe na nani ili muelewe”Alihoji
Mbunge Kitandula.
Mbunge
Kitandula alisema kwamba watu wa Mkinga waanasikitika sana na jambo
hilo huku aakieleza kwamba anataka kuweka rekodi sawa kwamba kuna maneno
yanasemwa kuwa watu wa Kaskazini wamependelewa jamani Tanga hatuna
barabara,Mkinga hatuna barabara huku Mkinga wana kilomita zisizozidi
kilomita 25 za lami ambazo zinakwenda mpakani Horohoro na hazikwenda
kwenye maeneo ya uzalishaji.
“Hebu
tutendeeni haki twendeni mkatusaidie kujenga barabara ya kutoka
Mabokweni ,Maramba,Mtoni Bombo,Mashewa kwenda Korogwe lakini tuunganishe
na barabaa ya kwenda Umba makutano mpaka Same”Alisema
Hata
hivyo alisema kwamba hivi sasa kwa upande wa wilaya ya Same Mkoani
Kilimanajaro upembezi yakinfu wa barabara hiyo umekamilika akahoji
kwanini kunakuwa kigugumizi kwa upande wa Tanga, hivyo wanamuomba Waziri
awaeleze kuhusu barabara hiyo
Akiendelea
kuchangia alisema kuna barabara imeanza kujengwa kwenda makao makuu ya
wilaya ya Mkinga lakini cha kushangaza na kichekesho wanajenga mita
200,mita 150 kwenye barabara yenye kilomita 48 akahoji tunapojenga hivi
tutamaliza lini; hivyo ninaiomba serikali ifikirie mambo hayo”Alisema
Mbunge Kitandula.
Mwisho.
Post A Comment: