Nteghenjwa Hosseah, Manyara


Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Grace Maghembe amesema kwa mwaka wa fedha 2020/21 wauguzi waliopo katika vituo vya kutolea huduma wamehudumia wagonjwa wapatao milioni 20 waliofika katika vituo hivyo kupata huduma mbalimbali za kiafya.


Dkt. Grace ameyasema alipokua akitoa salamu za Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Manyara.


Amesema wauguzi hao wametoa huduma za Nje yaani huduma za Mkoba kwa wananchi takribani milioni 1.2 ambazo zinahusisha zaidi huduma za mama na mtoto.


Aidha Dkt. Grace aliongeza kuwa wauguzi hawa wamezalisha wakina mama takribani laki moja na kutoa huduma dawa ya usingizi kwa wajawazito 25,000.


Dkt. Grace alibainisha mahitaji ya wauguzi wa sasa ni 41,000 lakini waliopo katika vituo vya kutolea huduma ni 19,000 ambapo ni sawa na asilimia 41 ya mahitaji.


Aidha, Dkt. Grace amesema kuwa ajira zilizotolewa kuanzia mwaka 2017/2019  ni 3,625  ambapo waliajiriwa na Serikali pamoja na wadau ambao ni Taasisi ya Benjamini.


" Na katika ya ajira 2,720 zilizotangazwa Mei 9 mwaka huu na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ajira za wauguzi ni 954 sawa na asilimia 35 ya ajira zote zilizotangazwa."


Amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Wauguzi na itanendelea kuboresha mazingira na utendaji kazi wao kadri rasilimali zinavyopatikana.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: