Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga Ndugu Saleh Mkwizu ameupongeza Uongozi wa Halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi wake Ndugu Zefrin Kimolo Lubuva Pamoja na Mkuu wa Wilaya Ndugu Thomas Apson ,kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016, 2016/2017, 2017/2018, 2018/2019 na 2019/2020.


Akizungumza nasi  mapema hii leo baada ya uwasilishaji wa hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Selikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Mwenyekiti huyo ameipongeza Halmashauri ya Mwanga kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo na kuwa Halmashauri ya pili Mkoani Kilimanjaro kwa ukusanyaji wa mapato katika Mkoa huo.

“Halmashauri hii ni ya mfano katika mkoa wa Mkoa wa Kilimanjaro hivyo niwaombe madiwani wenzangu sambamba na watumishi wote wa Halmashauri yetu haswa watu wa mapato ninawaomba msibweteke kwa vile mmepata mafanikio haya, bali muongeze bidii” alisema Salehe Mkwizu

 Hata ameendelea kueleza kuwa  mafanikio hayo ni matokeo mazuri ya Mkurugenzi wake Ndugu Zefrin Kimolo Lubuva ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Halmashauri inaendelea kupata hati safi akishirikiana sambamba na watumishi wa Halmashauri hiyo.

"Mshirikiano na uwajibikaji wa Menejimenti ndio umepelekea Halmashauri hii kuwa na hoja chache na kuwa na ufanisi,Mimi kama Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro niziombe Halmashauri zingine kuiga mfano huu” Saleh Mkwizu


Halmashauri ya Mwanga ilianzishwa Mwaka 1979 na kuanza kutekeleza majukumu yake halmashauri hii imekuwa chachu ya kuongeza tija kwa watendaji wote na hivyo kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma bora zinazotolewa katika sekta za afya, elimu, maji,miundombinu na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: