Mkuu wa Kampasi ya Karume- ZanIbar Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dkt Rose Mbwete amesema maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanatoa fursa kwa wanataaluma, wanafunzi na wanajamii kukutana kwa pamoja na kujadili fursa, changamoto zinazoikabili Jamii pamoja kupata uzoefu, ujuzi na maarifa kuhusiana na nafasi ya mwanamke katika uongozi na usawa katka kufikia malengo ya Taifa.


Dkt. Mbwete ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake lililoandaliwa na  Mtandao wa wanawake Viongozi Afrika - AWLN- tawi ka Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Cha  Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.


Amesema katika kukidhi takwa ka uswa wa kijinsia katika uongozi Chuo kimekuwa mstari wa mbele katika kuchangia juhudi za serikali katika masuala ya usawa wa kijinsia, ikiwa ni pamoja Chuo kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa kike katika fani mbalimbali.





Share To:

Post A Comment: